Visit Sponsor

Written by 7:02 pm BURUDANI Views: 34

BASATA WAGUSWA NA SHINDANO LA BSS

Na Beatrice Kaiza

BARAZA la Sanaa Taifa (BASATA) Lakiri kuguswa na juhudi zinazofanywa na Madam Rita kupitia shindano la Bongo star search (BSS) Kwa kuzalisha na kunyanyua vipaji vya vijana wengi chini kupitia Fani ya Muziki.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kutangazwa kwa fainali ya Shindano hilo, Afisa Mwandamizi (BASATA) Agustino Makame amesema kuwa baraza
linatambua mchango mkubwa unaofanywa na Shindano hilo katika kufufua, kukuza na kuwapa nafasi ya kutumia Jukwaa hilo kutimiza ndoto za Vijana wengi na hivyo kama Basata litakaa chini kuendelea kutoa ushirikiano kw Waandaaji hao.

Hata hivyo Makame amesema Waandaaji hao wamekuwa wakishirikiana na Basata tangu kuanza kwa mchakato wa awali hadi kuelekea kwa Fainali hiyo.

Mkurugenzi wa Masoko kutoka Startimes David Malisa amesema msimu huo wa 14 ulikuwa wa kitofauti kutokana na timu hiyo kufika Mji wa Kigoma na kupata writhing wengine wa Peter Msechu.

Aidha amesema wao Kama Startimes wataendelea kuunga Mkono Jitihada za Mama huyo kwa kuona ipo haja ya Jukwaa la BSS kutumika kwa Viiana hata walio Mikoani na kuwafikia kwa Lengo la kutimiza ndoto zao kupitia Muziki.

Pia Malisa amesema Fainali hizo zitarushwa mubashara kupitia St Swahili bila chenga ili kuwapa fursa ya kuwaona burudani mbalimbali usiku wa Kilele cha Fainali hizo.
“Kiingilio cha kawaida sh 15000, VIP 30,000 na WVVIP ni sh 50000. Hivyo kwa wale ambao hawajajiunga na familia ya Startimes wajiunge sasa ili wapate kushuhudia kila kitu.”

Kwa upande wake Jaji mkuu wa shindano hilo Rita Paulsen ameeleza utofauti wa Msimu wa 14 wa shindano hilo sababu kubwa akieleza kuwa vipaji vimekuwa vingi vizuri tofauti na misimu iliyopita na •kulazimika fainali kusindikizwa na sita bora (Top 06) baadala ya tano bora (Top 05) kama ilivyozoeleka.

“Msimu wa 14 viiana wamejitokeza wengi na mikoa mengine ilitulazimu tuchukue wat wengi na baadae tulipofanya mchuio tumebaki na na Viiana 06 ambao wamefanikiwa kuingia kwenye mchakato wa ushindani.”

Hata hivyo Paulsen ameweka wazi kuwa zawadi a Mshindi wa kwanza atapewa
Kiwania pamoja na pesa taslimu milioni 20, wakati mshindi wa pili atapewa milioni 3 huku washindi waliobakia wakipatiwa kifuta jasho Milion 1 kwa kila mmoja.

Pia ametoa wito kwa wizara husika pamoja na Baraza la sanaa Taifa (BASATA) kuweka nguvu kubwa kuwasaidia Waandaaji wa Bongo star search (BSS) Kutafuta wadau watakaoongeza nguvu kubwa kuhakikisha shindano hilo linafanyika kwa ufanisi mkubwa zaidi.

“Kiukweli tunahitaji nguvu kubwa mo katika shindano hili bado tunahitaji wadau tunaomba wizara husika watupe nguvu na waombe udhamini kwa Taasisi na Wizara mfano Wizara ya Utalii Inakuwa rahisi wenyewe kwa wenyewe wizara za serikali kusikilizana kwa haraka na kupatikana maribu kwa wepesi zaidi.”

About The Author

(Visited 34 times, 1 visits today)

Last modified: January 16, 2024

Close