Visit Sponsor

Written by 3:23 pm MICHEZO Views: 5

BARAZA LA MICHEZO UINGEREZA LAVUTIWA NA MANDELEO YA MICHEZO NCHINI

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu akiwa katika picha na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Uingereza Bi. Katherine Grainger baada ya kukutana na kufanya mazungumzo ambapo amesema wamevutiwa na maendeleo ya michezo nchini.

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amekutana na
kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Uingereza Bi. Katherine
Grainger ambapo amesema wamevutiwa na maendeleo ya michezo nchini.

Kikao hicho cha Viongozi hao kimefanyika Juni 27, 2023 jijini Dar es Salaam ambapo
wamejadili namna Tanzania na Uingereza kuimarisha ushirikiano katika michezo ambao ni wa kihistoria.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wamejikita katika maeneo ya ushirikiano baina
ya nchi hizo mbili katika mafunzo ya michezo ambayo yametekelezwa kwa kipindi cha
zaidi ya miaka 10 iliyopita tangu 2012 wakati Uingereza ilipokuwa inaandaa
mashindano ya Olympic ambapo walifundisha walimu wa michezo na kuhimiza watu
kushiriki katika michezo.

Matokeo baada ya himizo hilo, michezo ya marathoni iliongezeka Tanzania kutoka
mashindano mawili mpaka 126 ambayo yapo hadi sasa, michezo ya jogging na
kuongezeka kwa idadi ya makocha ambao sasa wanafundisha ligi mbalimbali nchini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Uingereza Bi. Katherine
Grainger amesema wataendelea kuimarisha ushirikiano na Tanzania katika sekta ya
michezo hasa mchezo wa Skateboard ili kuendeleza wanamichezo wa mchezo huo
kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa.

Aidha, Uongozi wa Chama cha Skateboard cha Uingereza, wapo hapa nchini kutoa
mafunzo kwa kushirikiana na Chama cha Skateboard cha Tanzania ili kuimarisha na
kuendeleza mchezo huo.

About The Author

(Visited 5 times, 1 visits today)

Last modified: June 27, 2023

Close