Bandari ya Dar es Salaam imefikia rekodi ya kihistoria kwa kuhudumia zaidi ya tani milioni 18 za shehena hadi kufikia Mei 2023. Muda wa kuhudumia shehena umepungua sana na sasa unachukua chini ya siku nne.
Mkakati wa maboresho na ujenzi wa miundombinu katika bandari hiyo umesaidia kuongeza ufanisi na kuboresha huduma za bandari. Kina cha maji kimeongezeka kutoka mita 6-7 hadi mita 14.5, na kujenga magati mapya imefanya bandari hiyo kuwa na uwezo wa kuhudumia meli kubwa zaidi.
Bandari ya Dar es Salaam sasa inapokea idadi kubwa ya meli kubwa (Deep sea vessel), na watumiaji wa bandari wameongezeka kwa kiasi kikubwa. Pia, kumekuwa na maboresho katika huduma za usafirishaji wa magari, na bandari hiyo ina gati maalum kwa kuhudumia shehena ya magari.
Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho, amesisitiza umuhimu wa ushiriki wa sekta binafsi katika uendeshaji wa bandari na kuwahimiza watumiaji wa bandari kutumia bandari za Tanzania kwa sababu ya usalama, unafuu wa gharama, na ufanisi wa huduma.
Bandari ya Dar es Salaam ni kiungo muhimu cha biashara kwa Tanzania na nchi jirani, na inahudumia biashara ya kimataifa kwa nchi za Afrika Mashariki, nchi za Mashariki ya Kati, Mashariki ya Mbali, Ulaya, Australia, na Marekani.
About The Author
Last modified: May 29, 2023