Mbunge wa Morogoro Vijijini, Hamis Tale Tale maarufu kama Babu Tale amewashika mkono wafanyabiashara wadogo wanaofanya shughuli zao pembezoni mwa barabara eneo la Mikese kwa kuwajengea vibanda vya kisasa.
Akiongea na mwandishi wa habari hii leo Machi 8, 2024 mbunge huyo amesema kuwa amefanya uamuzi huo wa kuwajengea vibanda vya biashara katika muundo wa kisasa ili kuongeza thamani ya shughuli zao na kuhifadhi biashara zao katika hali ya usalama.
![](https://www.mwanahabaridigital.co.tz/wp-content/uploads/2024/03/6-1-1024x568.jpg)
“Tunaifanya imani kuwa thabiti, kwa maana imani iko katika matendo.
Nimepata nafasi ya kukutana na ndugu zangu wa Kitongoji cha Fulwe Kata ya Mikese, nimefanya uamuzi wa kuwatengenezea vibanda vya biashara katika muundo wa kisasa,” amesema Babu Tale.
Aidha Tale amesema kuwa wanaijenga imani yao kwa kuyagusa waliyonayo kwani huo ndio muelekeo wa Serikali ya Awamu ya Sita.
![](https://www.mwanahabaridigital.co.tz/wp-content/uploads/2024/03/2-1024x571.jpg)
About The Author
Last modified: March 8, 2024