Visit Sponsor

Written by 10:25 am BURUDANI Views: 17

AZAM WAZINDUA TAMTHILIYA MBILI KWA MPIGO

Na Beatrice Kaiza

Azam Tv wamezindua tamthiliya mbili ya Koneksheni inayotarajiwa kuanza tarehe 6 mwezi 5 (jumatat -alhamis) na Mawio inayotarajiwa kuanza tarehe tarehe 7 mwezi 6(ijumaa-jumapili) mwaka huu katika kisimbuzi Cha azam Tv channel ya Sinema zetu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam, Msimamizi mkuu wa chaneli ya Sinema zetu, Sophia Mgaza amesema tamthiliya hizo zinalenga kuleta Mapinduzi katika tasnia ya filamu nchini.

Mgaza ameleza kuhusu Tamthiliya ya Mawio ambapo alisema “Hadithi inayomhusu Hamadi, kijana wa Zanzibar anayeishi Unguja, ambaye aliamua kuoa mara ya pili kwa siri huku mke wake wa kwanza akiwa hajui lolote.

Isivyo bahati, dakika chache baada ya kufunga ndoa, inagundulika kuwa mke aliyemwoa ni mke halali wa rafiki mkubwa wa kaka yake ambaye ni kigogo serikalini. Hivyo analazimika kuachana na mkewe siku hiyo hiyo aliyomuoa, hali inayosababisha vyombo vyote vya habari vya Unguja kuripoti suala hilo la kipekee.”

Mgaza aliendelea kueleza kuwa “Taarifa hizi zinamfikia mke wake mkubwa ambaye ni mwanamuziki maarufu wa Taarabu mjini Unguja ambaye anaamua kulipiza kisasi kwa kuanzisha mapenzi na mtalii kutoka Marekani kutokana na hasira za kusalitiwa na mumewe.

Wawili hawa wanaamua kukimbilia kisiwa jirani cha Lamu na kuanza maisha mapya Je huko ni kinaendelea; usikose kukutana nasi sebuleni kwako kuoitia chaneli namba 103.”

Mgaza amesema Tamthilia6 hiyo imesheheni mastaa wengi ambao hukuwahi kuigiza sehemu yoyote isipokuwa katika tamthilia hii ya Mawio, mastaa hao ni pamoja na Elias Inyasi (Barnaba Classic), Isha Makongoro (Isha Mashauzi, Maisala Abdu Shamte (Uncle Shamte), Patricia Hilary, Rushay na Salum, Mario Jose Martos (Raia Hispania Yulia Babystrukova (Raia wa Siberia – Urusi) Licha ya mastaa hawa, wasanii wengine waliocheza katika tamthilia hii ni pamoja ‘Salim Ahmedy (Gabo), Yobnesh Yusuph (Batuli actress), Abdulrahman Mwita (Ray Coconut), Halima Yahya, Zainab Mbaruk (Zai Kijiwe Nongwa), na Single Mtarnbalike (Richie Richie)

Kuhusu Tamthiliya ya Koneksheni, Mgaza
ni hadithi inayohusu usaliti wa wanandoa katika ndoa.

Amesema Katika tamthilia hii tunamwona Kijo (mtu mwaminifu katika ndoa yake akisalitiwa na mkewe Jasmin). Usaliti wa Jasmin unapelekea Kijo kupewa mtoto (Anna) ambaye sio damu yake. Kijo baada ya kugundua mwanaume ambaye ana mahusiano na mkewe (Salim) anaamua kumteka kwa lengo la kumfundisha adabu ili aache kutembea na wake za watu, lakini anatambua kuwa uhusiano.

(Visited 17 times, 1 visits today)

Last modified: May 3, 2024

Close