Visit Sponsor

Written by 12:17 pm BURUDANI Views: 24

AZAM MEDIA YAZINDUA MFUMO MPYA WA KUPOKEA TAMTHILIA

Na Beatrice Kaiza

KAMPUNI ya Azam Media imetambulisha mfumo mpya wa upokeaji wa kazi za tamthilia za kitanzania zinazoruka kwenye Chaneli ya Sinema Zetu kuepuka wizi wa kazi za Sanaa.

Akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam, msimamizi Mkuu wa Chaneli ya Sinema Zetu, Sophia Mgaza wakati wa uzinduzi wa mfumo huo mpya amesema kuwa uzalishaji wa tamthia hiyo umezingatia mahitaji ya soko kwani wametumia vifaa vya uzalishaji wa kisasa na ubora wa hali ya juu,” amesema Mgaza.

“Kuanzia leo tutaanza kupokea filamu mlizoziandaa” ameyasema hayo Mgaza wakati akitangaza kufunguliwa kwa dirisha la filamu kupitia wavuti maalum ya “Azam TV Content Portal”

Mgaza amezungumza hayo wakati wa uzinduzi
wa tamthilia mpya ya Toboatobo itakayoanza
Februari 09, 2024.

“Awali walikuwa unapeleka demo kwanza kwa sasa hali imekuwa nitofauti unatakiwa kuingia mtandaoni kujisajili na kujaza fomu na kuweka mikataba mbalimbali ikiwemo mwandishi wa stori vibali vya Cosota,” amesema Mgaza.

Ameongeza kuwa waandaaji wapya wanaongia na kazi zao za sanaa zinazoruka kwenye chaneli hiyo kuhakikisha wanasimamia ubora wa kazi ili wasije kutoa sababu kwa watu wa pembeni kuwanyooshea vidole na kusema kuwa ilikuwa ni nguvu ya soda tu,” amesema Mgaza.

(Visited 24 times, 1 visits today)

Last modified: February 3, 2024

Close