Visit Sponsor

Written by 12:31 pm KITAIFA Views: 43

AWESO ATEKELEZA MAELEKEZO YA WAZIRI MKUU, AGAWA PIKIPIKI KWA WANUFAIKA LINDI

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso anaeendelea na ziara ya kikazi mkoani Lindi katika kukagua na kusimamia utekelezaji wa Miradi ya Maji ameanza kwa kutekeleza maagizo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa alioifanya tarehe 08 January 2024 Lindi.

Waziri Aweso alianza kazi hiyo kwa kumaliza usajili wa pikipiki zilizokaa muda mrefu kutokana na uzembe wa watendaji na rasmi amegawa pikipiki hizo kwa wanufaika.

Akiwa na viongozi wa Mkoa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Zainab Telack amegawa jumla ya Pikipiki 22 kwa CBWSO 19 kwa ajili ya usimamizi na uendeshaji wa skimu za Maji vijijini,

Lengo kuu la kugawa pikipiki hizo ni kurahisisha utendaji kazi wa CBWSO’s kutokana na ukubwa wa maeneo ya kutolea huduma.

About The Author

(Visited 43 times, 1 visits today)

Last modified: January 27, 2024

Close