Kamanda Kanda Maalum Dar es salaam, SACP Jumanne Muliro akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani), Dar jana
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linawashikilia askari 6 wa jeshi hilo na walinzi 11 wa kampuni ya ulinzi ya Pasco Ltd pamoja na maafisa misitu wawili wakituhumiwa kusababisha vifo vya watu wawili maeneo ya Kiluvya, Dar es salaam Agosti 28, 2023.
Akizungumza na Wandishi wa Habari leo Agosti 29, 2023, Kamanda Kanda Maalum Dar es salaam, SACP Jumanne Muliro amesema tukio hilo lilitokea usiku wakati maafisa hao wakitimiza majukumu yao ya kuhakikisha mazao ya misitu inalindwa na wanaofanya biashara hizo wanafuata taratibu ndipo wauza mkaa 30 wakakimbia na kuacha pikipiki zao.
“Baada ya muda kidogo walirudi na kuanza kuwarushia mawe maofisa na makamanda wa polisi wakaanza purukushani.”alisema Muliro na kwamba miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Mloganzira na silaha zote zimechukuliwa kwa ajili ya uchunguzi.
Watuhumiwa wote wanashikiliwa na jeshi la polisi na uchunguzi bado unaendelea.
About The Author
Last modified: August 29, 2023