Visit Sponsor

Written by 1:06 pm BIASHARA Views: 3

AIRTEL YAZINDUA TEKNOLOJIA YA AKILI MNEMBA KWA KUWAKOMESHA MATAPELI

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM MWANAHABARI

Airtel Tanzania imezindua huduma maalum ya kutoa taarifa kuhusu utapeli kupitia Akili Mnemba ya ambayo imetengenezwa mahususi kwa ajili ya kuwatahadharisha wateja dhidi ya ulaghai na utapeli ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuongeza hatua za kupambana na uwepo wa utapeli kwa njia ya simu nchini Tanzania.

Ameyasema hayo Leo 28 April 2025 akizungumza wakati wa uzinduzi, Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa ameipongeza Airtel kwa kutengeneza teknolojia ya kibunifu nchini akiongeza kuwa huduma hiyo ya kimapinduzi ya Airtel Spam Alert Service-Kataa Matapeli itakuwa na mchango muhimu katika kuunga mkono jitihada za serikali kutatua utapeli nchini Tanzania.



“Huduma ya Airtel Spam Alert-Kataa Matapeli, inayotumia Akili Bandia kugundua ulaghai mtandaoni, inaendana moja kwa moja na juhudi za serikali kuhakikisha wananchi wanakuwa salama na wanaweza kuepuka matapeli wa simu kwa haraka zaidi,” Amesema Silaa

Aidha Silaa amesisitiza kuwa hatua iliyochukuliwa na kampuni ya simu inaendana na kampeni inayoendelea ya kitaifa dhidi ya udanganyifu wa simu za mkononi iitwayo #Sitapeliki, inayolenga kuelimisha umma na kuwawezesha kutambua na kuepuka matapeli wa simu.



Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Charles Kamoto, amesema kuwa suluhisho hili la kisasa la AI ni uthibitisho wa dhamira ya Airtel kuwawezesha wateja wake dhidi ya vitisho vinavyotokana na matapeli wa simu za mkononi, na kwamba huduma ya Airtel Spam Alert-Kataa Matapeli inapatikana kwa watumiaji wote wa simu janja na simu za kawaida.

“Huduma ya Airtel Spam Alert-Kataa Matapeli tayari inapatikana kwa wateja wote wanaotumia simu janja au simu ya kawaida, na muhimu zaidi, wateja wetu hawatahitajika kupakua programu yoyote au kufuata hatua za kuiwasha. Hii si tu tangazo la teknolojia kuhusu hatua muhimu ya kulinda wateja, bali ni tamko kwamba Airtel Tanzania si mtandao wako tu, bali pia ni mlezi wako wa kidijitali. Tumejitoa kikamilifu kuwawezesha wateja wetu kuwa makini na kuwapa imani ya kufurahia manufaa ya mawasiliano ya kidijitali,” Amesema Kamoto



Kamoto pia alitoa wito kwa wadau wa sekta ya mawasiliano kuunga mkono juhudi zinazolenga kukabiliana na udanganyifu wa simu katika jamii.

Kuanzishwa kwa huduma ya Airtel Spam Alert-Kataa Matapeli nchini Tanzania inafuatia mafanikio ya uzinduzi wa teknolojia hiyo ya Akili Mnemba nchini Nigeria na Uganda wakati kampuni hiyo ya mtandao wa simu inavyoendelea kuboresha uzoefu wa wateja kwa kuwa huduma hiyo itakuwa inapatikana kwenye simu janja na simu za kawaida zote kwa ajili ya jumbe zinazoshukiwa kuwa za kitapeli. Haihitaji kupakua aplikesheni kwa kuwa inapatikana kwa wateja wote wa Airtel.

About The Author

(Visited 3 times, 3 visits today)

Last modified: April 28, 2025

Close