Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI
Msimu wa tatu wa Tamasha la Mtoko wa Pasaka umekuwa wa aina yake kutokana na wasanii wa injili kutoka ndani na nje ya nchi kulipambana tamasha hilo.
Kila msanii anayepanda jukwaani ukumbi unalipuka kwa shangwe na baadhi ya washiriki wanashindwa kujizuia na kuamua kusimama kucheza na kuimba.

Baadhi ya wasanii kama vile Christopher Mwahangila, Solomoni Mukubwa kutoka Kenya na wengine wamenogesha tamasha hilo kwa aina ya uimbaji waliouonyesha na nyimbo mbalimbali ambazo zinapendwa na Watanzania wengi.Mbali ya wasanii hao Kwaya ya Mtakatifu Kizito – Makuburi nayo imekuwa kivutio kikubwa hasa kupitia nyimbo zake kama vile Haleluya Kuu na Msalaba ambazo zimewainua washiriki na kuimba pamoja.

Tamasha hilo lenye kaulimbiu ‘Kwa maombi tutashinda’ linaendelea katika ukumbi wa The Super Dome Masaki, Dar es Salaam.
About The Author
Last modified: April 20, 2025