Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI
KUHUDHURIA kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM), Balozi Emmanuel Nchimbi katika tamasha la Pasaka ‘Mtoko wa Pasaka’ imeelezwa kuwa ni kilelezo kuwa chama hicho kipo karibu na wasanii nchini wakiwemo wa nyimbo za Injili.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto amebainisha hayo leo Aprili 20, 2025 kwenye tamasha hilo ambalo pia limetumika kumuombea dua Rais Samia Suluhu Hassan.
“Katika tamasha kuhudhuria kwa Balozi Nchimbi inadhihirisha namna chama kilivyokuwa karibu wasanii na hii inaleta umoja na mshikamano katika nchi yetu.
Nimshukuru katibu mkuu wetu wa Chama Cha Mapinduzi, Dkt Emmanuel Nchimbi Kwa kukubali waliko huu inaonesha namna Serikali ya Awamu ya Sita ilivyokaribu na wasanii,” amesema.
Tamasha hilo la Mtoko wa Pasaka wasanii wa nyimbo za Injili wa kitaifa na kimataifa ambao Kwa muda tofauti walipata nafasi ya kutoa burudani.
Ameongeza kuwa kufanyika kwa tamasha hilo pia kunaongesha ‘connection’ baina ya wasanii kwa wasanii na wasanii na viongozi na kusaidia kuwaweka pamoja.
About The Author
Last modified: April 20, 2025