Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM MWANAHABARI
Taasisi isiyo ya kiserikali iliyosajiliwa na inayo fanya kazi za hisani Tanzania bara na Zanzibar JAMIIBORA HEALTH SERVICES NETWORK inashirikiana na wadau wengine Kwa kuandaa kongamano la kwanza la magonjwa ya mfumo wa Chakula litakalofanyika siku ya 24 Mei 2025 Katika ukumbi wa mikutano wa ummy mwalimu Katika hospital ya muhimbili.
Kongamano hilo linawaleta pamoja wataalumu mbalimbali wa afya wenye hamasa ya kujifunza na kujadili maendeleo ya hivi karibuni pamoja na mwelekeo wa matibabu Kwa wagonjwa wenye matatizo ya mfumo wa Chakula
Ameyasema hayo 15 April 2025 Katibu Mkuu Jamiibora Hearth service network Dr Muhidin Mahende Amesema Tukio hilo litajumuisha mada zitakazowasilishwa Moja Kwa Moja,Majopo ya mijadala ya kina,na vipindi vya maswali na majibu Kuhusu mada kuu mbalimbali zinazohusu masuala ya mfumo wa Chakula
“Tunawaalika wataalumu wa mfumo wa Chakula, wataalumu wengine wa Tiba na afya shirikishi, wanafunzi wa kozi mbalimbali za Afya, wafanyakazi wa vyuo vikuu, wafanyakazi wengine wa hospital,wamiliki wa hospital, wasambazaji wa dawa na vifaa Tiba,wasimamizi na waratibu wa huduma za Afya,vyama vya kitaaluma vya tiba na sayansi shirikishi, taasisi za serikali pamoja na wananchi Kwa ujumla kuhudhuria kongamano hili muhimu”Amesema Mahende
Pia Mahende Amefafanua kuwa Tukio hilo linatarajiwa kufanyika Kwa mfumo wa aina 2,Kwa njia ya ana Kwa ana na mtandaoni,Ili kuruhusu ushiriki wa watu walioko nje ya dar es salaam na kutoka sehemu mbalimbali Duniani kuwa sehemu ya tukio muhimu
“Njia za wavuti za usajili pamoja na zile za kushiriki mtandaoni zitatolewa Kupitia tovuti rasmi ya tukio https://www.teagic.africa/ pamoja na kwenye mitandao yetu mbalimbali ya kijamii ya taasisi ya Jamiibora”.ameendelea kufafanua Mahende
Mahende Amesema tunawaalika wote kuhudhuria tukio hilona pia tunawakaribisha ushiriki wenu
Kauli mbiu ya kongamano hilo ni: ” Kuendeleza sayansi ya magonjwa ya mfumo wa Chakula Africa mashariki: Ubunifu, changamoto na mwelekeo wa baadaye”.
About The Author
JAMIIBORA HEALTH SERVICES NETWORK
Last modified: April 15, 2025