Visit Sponsor

Written by 6:45 pm KITAIFA โ€ข Views: 6

DKT. BITEKO ATAKA WANANCHI WAPEWE MAJIBU YA HUDUMA KWA HARAKA NA HAKI



๐Ÿ“Œ Aipongeza EWURA kwa taarifa yenye mchango muhimu kuimarisha sekta ya nishati

๐Ÿ“Œ Vyombo vya moto vinavyotumia gesi vyaongezeka kufikia 7,000

๐Ÿ“Œ Mahitaji ya umeme kufikia megawati 8,055 mwaka 2035

๐Ÿ“Œ Upatikanaji wa mafuta waendelea kuimarika nchini

๐Ÿ“Œ TANESCO yaendelea kuimarika na kupata faida

Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka watendaji wa sekta ya nishati kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kutoa huduma bora kwa wananchi.

Pia, ameipongeza  Bodi ya Wakurugenzi na Wafanyakazi EWURA kwa uandaaji wa Taarifa za Maendeleo ya Sekta ya Nishati kwa Mwaka 2023/24 kwa kuwa  zina umuhimu mkubwa kwa Serikali katika kufanya maamuzi, kwani zinasaidia kuona mwenendo wa sekta ya nishati kwa  kuonesha  hali ya sekta hiyo  ya nishati, mafanikio, changamoto na fursa zilizopo katika kuiendeleza.

Dkt. Biteko ameeleza hayo leo Aprili 9, 2025 jijini Dodoma wakati aliposhiriki katika uzinduzi wa Taarifa za hizo Maendeleo ya Sekta ya Nishati kwa Mwaka 2023/24.

โ€œ Wananchi wapewe majibu ya haraka na ya haki, taarifa hii imeonesha bado tuna kazi kubwa ya kufanya. Tunachotaka ni Watanzania kupata huduma iliyo bora na hiyo itasaidia kutokuwa na malalamiko ya upatikanaji wa huduma kutoka kwa wananchi,โ€ amesema Dkt. Biteko.

Amesema kuwa Serikali inaendelea kujenga vyanzo vipya vya umeme na kuweka msukumo mkubwa katika uwekezaji wake ili kukabiliana na hatari ya uhaba wa umeme inayoweza kutokea zisipofanyika jitihada za makusudi na za haraka.

โ€œMahitaji ya umeme yameongezeka hadi megawati 254 ambapo ni sawa na kujenga mradi mwingine kama wa Kidatu, ifikapo mwaka 2030 mahitaji ya juu ya umeme yatakuwa megawati 4,878 na mwaka 2025 mahitaji ya juu ya umeme yatafikia megawati 8,055 taarifa hii inaonesha hatari kama hatutachukua hatua,โ€ amebainisha Dkt. Biteko.

Kwa upande wa sekta ndogo ya gesi asilia, Dkt. Biteko amesema  kama zilivyo sekta nyingine za nishati kwa mujibu wa Taarifa hiyo, imeonesha kuwepo ongezeko la matumizi ya gesi asilia viwandani, majumbani na kwenye vyombo vya usafiri. Aidha, vituo vya kujaza gesi iliyoshindiliwa kwenye magari (CNG) vimeongezeka.

Kuhusu mafuta amesema  taarifa hiyo  inaonesha kuimarika kwa upatikanaji wa mafuta nchini pamoja na jitihada za kuhamasisha wawekezaji wa ndani kujenga vituo vya mafuta katika miji midogo na vijijini ili kuongeza wigo wa upatikanaji wa bidhaa hiyo. Aidha, amezipongeza kampuni za mafuta kwa kushirikiana vizuri na Serikali.

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amesema pamoja na jitihada za Serikali kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika ya umeme, mafuta na gesi asilia bado sekta inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwepo mabadiliko ya tabia nchi na uharibifu wa mazingira, upungufu na uchakavu wa miundombinu.

Ametaja changamoto zingine ni za rasilimali fedha kwa ajili ya uwekezaji na za maendeleo ya sayansi na teknolojia. Hata hivyo, ili kuondokana na changamoto hizo amesema , Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine, itaendelea kuhakikisha inaboresha, inaimarisha, inarahisisha na inawezesha upatikanaji wa nishati safi kwa Watanzania wote.

โ€œ Namshukuru sana na kumpongeza Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa mchango mkubwa katika kuimarisha sekta ya nishati. Chini ya uongozi wake, tumeshuhudia maendeleo makubwa katika sekta hii ikiwemo ukamilishwaji wa miradi mikubwa ya kimkakati na kielelezo ambayo imeongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini, upatikanaji wa bidhaa za petroli, pamoja na ongezeko kubwa la matumizi ya gesi asilia hususani kwenye magari,โ€ amesisitiza Dkt. Biteko.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Wizara ya Nishati, Mhe. Judith Kapinga โ€œNaendelea kumpongeza Rais Samia kwa kazi kubwa inayofanyika katika sekta ndogo ya nishati, na usimamizi mzuri wa Dkt. Biteko unaowezesha kupata mafanikio yote haya,โ€ ameeleza Mhe. Kapinga.

Naye, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi EWURA, Prof. Mark Mwandosya ameishukuru na kuipongeza Serikali kwa uwekezaji mkubwa inaoendelea kuufanya katika sekta ya nishati.

โ€œ Hii miradi mikubwa hasa ya umeme mfano Bwala la Julius Nyerere inachukua muda mrefu hadi kukamilika kwake hivyo ni kiashiria kwamba tuanze sasa kutekeleza miradi mingine ili baada ya miaka kadhaa tusijekupata changamoto ya umeme,โ€ amesema Prof. Mwandosya.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA), Dkt. James Andilile amesema kuwa uzinduzi wa taarifa hizo ni takwa la kisheria na tayari wameshafanya hivyo kwa upande wa sekta ya maji.

Amesema katika sekta ndogo ya umeme hadi kufikia Juni 2023/2024 uzalishaji wa umeme ulikuwa megawati 2,411 na sasa umefikia megawati 4,032.

โ€œKutokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa umeme huduma imeimarika na sasa changamoto iliyokuwepo imeondolewa. Kuhusu gharama za bei ya umeme kutokana na uwekezaji katika miundombinu hali ya fedha TANESCO imeendelea kuimarika na mwaka wa tatu mfululizo imetengeneza faida kutokana na usimamizi wa Serikali wa kuondokana na mitambo ya kukodi ya kuzalisha umeme,โ€ amesema Dkt. Andilile

Ameongeza kuwa katika sekta ya mafuta hadi kuishia Juni 2023/2024 vituo vya mafuta vilikuwa 2,361 sawa na ongezeko la asilimia 10, kukiwa na vituo 480 vijijini sawa na ongezeko la asilimia 12. Pia, kuhusu gesi asilia amesema  katika mwaka 2020/2023 vyombo vya moto vilivyokuwa vinatumia gesi asilia vilikuwa 7,000  na kufikia Machi mwaka huu vimefikia 15,000 ikiwa ni sawa na asilimia 49.

About The Author

(Visited 6 times, 1 visits today)

Last modified: April 9, 2025

Close