Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM MWANAHABARI
Waziri wa Elimu Adolf Mkenda Amepongeza Bodi ya Tume ya Nguvu ya Atom TAEC Kwa kutenga Bajeti iliyoelekezwa na serikali Kwa ajili ya kwenda kuwafundisha Watanzania nje ya nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari Leo 19 Frebuari 2025 jijini dar es salaam wakati akizindua Bodi ya Tume ya Nguvu ya Atom TAEC Waziri wa Elimu Adolf Mkenda Amesema serikali imetenga fedha Kwa ajili ya Mafunzo ya Muda mrefu ya vyuo vikuu nje ya nchi
Amesema kuwa Samia Scholarship Extended ni Kwa ajili ya kuwapeleka watanzania kwenda kusoma kwenye vyuo Bora kabisa hapa dunia kwenye mambo ya Atom,Nyuklia Kwa ajili ya kuendeleza fani hapa nchini

“Tanzania Katika eneo hili lipo vizuri sana kuliko nchi nyingine na wageni wanakuja hapa,lakini tunasema Bado tunauhitaji wa kwenda umbali zaidi,sisi tunamadini ya Uraniam lakini Kuna probability nyingi tu lakini hatujazi kutumia vizuri,maswala ya tiba Kwa kutumia nishati ya Atom (Miyozi),na halikadhalika na mambo ya kilimo,Tunaitaji kuwa na nguvu kubwa”Amesema Mkenda
Pia Waziri Mkenda Amesema swala la scholarship ya kwenda nje mara nyingi ni la serikali japo nchi nyingi zipo tayali kukupa msaada ila kutoa scholarship sio common sana.
Mkenda ametoa angalizo Kwa Tume.”Twendeni tukajifunze Katika vile vyuo Bora ambavyo mulivyonionesha wenyewe tukawapeleke watanzania wakasome Kwa Bajeti hiyo na mliyoitenga,Kwa hili Bodi ningependa liendelee na mlisimamie”Amesisitiza Mkenda

“Na tunawapa final disisheni na hamna haja ya kuja wizarani nyie sio Idara ya wizara ya elimu sayansi na teknolojia nyie ni taasisi ambayo inayofanya kazi, Bodi hiyo inayofanya kazi Kwa niaba yetu sisi,tunawapeni mamlaka ya kuchagua na kuwapeleka kulingana na sisi miongozo tuliyoitoa”
Aidha Amesema tunawapa kipaumbele Tume yetu ya ndani Kwa usajili huo wa mastazi au Phd kwani hatuwezi kuwaacha watu Wetu wa ndani,pia Kwa vyuo vikuu Kwa wale wanaouhitaji Kwa kuwaendeleza Kwa kuwatumia vizuri kwani Bajeti ipo watanzania wakasome
Nae Mwenyekiti wa Bodi ya TAEC Joseph Msambichaka amemshukuru RAIS samia Kwa kuweza kumchagua Katika Tume hiyo ya ukurugenzi wa Bodi ya TAEC
About The Author
Last modified: February 19, 2025