Visit Sponsor

Written by 4:03 pm KITAIFA Views: 3

RC CHALAMILA ATAKA JAMII KUTAFSIRI KWA VITENDO MAENDELEO YANAYOFANYWA NA RAIS SAMIA



-Asema kwa mfano Rais Dkt Samia ameboresha kwa kiasi kikubwa sekta ya elimu Je? jamii na wadau wengine wa elimu wanafanya nini ili kuinua viwango vya ufaulu.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila amewataka viongozi na wataalamu Mkoani humo kutafsiri vema na kwa vitendo maendeleo yanayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya elimu na afya ili iwe na tija kwa jamii hususani katika kuinua ufaulu wa wanafunzi kwenye shule ambazo hazifanyi vizuri

RC Chalamila akizungumza leo Feb 10, 2025 Wilayani Temeke Jijini Dar es salaam katika mkutano na wadau mbalimbali wa elimu amesema Serikali chini ya Rais Dkt Samia imekuwa ikiimarisha miundombinu ya elimu na mazingira ya kufundishia na kujifunzia hivyo ni muhimu kwa kila mdau wa elimu ikiwemo wazazi, viongozi pamoja wataalamu kujielekeza kwenye kusaidia watoto ili kuinua viwango vya ufaulu kwa wanafunzi

Aidha RC Chalamila amesema kuwa badala ya kutazama sababu chache zinazotolewa na kuonekana kusababisha ufaulu kuwa hafifu ni muhimu kufanya utafiti wa kina na kuhakikisha wazazi wanashirikishwa ipasavyo kwenye kuinua ufaulu wa wanafunzi ili  ndoto za Rais Dkt Samia zitimie na fedha nyingi anazozitoa kuimarisha miundombinu ya elimu zitimize lengo husika.

Vilevile RC Chalamila amesema hivi karibuni Serikali Mkoani humo inatarajia kufanya mkutano utakaojumuisha wazazi na wadau wengine wa elimu ili kujadili kwa pamoja na kuimarisha ushirikishwaji wa wazazi kwenye masuala ya elimu.

Naye Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe Sixtus Mapunda amesema wanakwenda kujielekeza kwenye kutafuta chanzo cha changamoto ya wanafunzi kutofanya vizuri kwenye mitihani yao ili kupata suluhisho la kudumu kwenye elimu na kwamba pamoja na kuendelea kuimarisha miundombinu watashirikisha wazazi  na wahitimu wa vyuo vikuu kwenye kada ya elimu

Sanjali na hilo mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke Abdallah Mtinika ametaja changamoto ya lugha ya kingereza kama kikwazo cha ufaulu kwa wanafunzi huku Afisa elimu Mkoa wa Dar es salaam Bwana Gift Kyando akizungumzia changamoto ya usafiri kwa wanafunzi wanaosoma shule za mbali ambao wamekua wakiachwa vituoni na magari.

About The Author

(Visited 3 times, 1 visits today)

Last modified: February 10, 2025

Close