Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI
• Dkt. Samia Suluhu Hassan – Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
• Dkt. Emanuel Nchimbi – Mgombea Mwenza
• Dkt. Hussein Mwinyi – Mgombea Urais wa Zanzibar
Katibu wa NEC, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla, amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitatumia maadhimisho ya miaka 48 kuwatambulisha rasmi kwa wanachama wake wagombea wa nafasi za urais.
Dkt. Samia Suluhu Hassan atatambulishwa kama mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Hussein Mwinyi kama mgombea urais wa Zanzibar, na Dkt. Emanuel Nchimbi kama mgombea mwenza.
Makalla ameyasema hayo leo, Jumatatu, tarehe 3 Februari 2025, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa NEC (White House), jijini Dodoma.
Aidha, amesema mgeni rasmi katika maadhimisho haya atakuwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Wanachama wa CCM wamekaribishwa kuhudhuria kwa wingi katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, ambapo mageti yatafunguliwa kuanzia saa 12 asubuhi.
About The Author
Last modified: February 4, 2025