Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM MWANAHABARI
NewTan Insurance imeleta mabadiliko Kwa wateja wao wa bima Kwa kuwapa elimu ya bima Kwa wakulima ambao ni watumiaji wa bima hiyo Kwa ajili ya kuweza kujikinga na majanga ambayo yatakayoweza kujitokeza Katika kilimo
Hayo Ameyasema Leo Tarehe 21 January 2025 Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa NewTan Insurance Nelson Rwihula Amesema Katika kilimo Kuna majanga mbalimbali yanayoweza kutokea,Kuna majanga ya Zao la Tumbaku,Mvua ya mawe, majanga ya mafuriko ambayo sio yanayoweza kuharibu mazao tu inaweza kutoa mbolea ambayo iliyowekwa na mazao yasikue yanavyopatikana
“Kuna majanga mkulima anakuwa nayo kila siku na majanga ya magonjwa ambayo hayazuiliki na wadudu ambao hawazuiliki na ukame,Sasa bima ya kilimo inacaver vitu vyote”,
“Mvua haIjanyesha na umepanda mpunga naunategemea Mvua zinakuja utavuna Mvua zisipokuja,umepanda mazao mbalimbali Kuna ukame Kuna wadudu Kuna magonjwa Sasa bima inakuja hapo kuangalia je kama usipopata majanga ungeweza kuvuna kiasi gani, kwenye shamba Moja unatarajia kupata magunia 50 tunakuja kuangalia kwenye hilo shamba la heka 50 umepata magunia 5,sisi tunaangalia Ile hasara uliyoipata tunakuja kucaver tunakuja kukulipa magunia yako 45 yaliyopotea”. Amesema Rwihula
Nae Meneja wa biashara za Benki NewTan Insurance Frank Kajo Amesema kama serikali inavyohimiza Zaidi Kwa wakulima kuwa kwenye vikundi Kwa maana ya ushirika Ili iweze kuwafikia Kwa urahisi Kwa mahitaji mbalimbali na sisi tunaungana na serikali Katika nyanja hiyo Kwa kuwafata wakulima kwenye vikundi vyao
Kajo Amefafanua Kuna kunamazao mengi kulingana na wizara ya kilimo inavyotoa Kwa wahusika na linalimwa Kwa wakati Gani na msimu Gani,miongozo IPO kutoka Katika mamlaka ya bima Katika Kampuni za insurance yeye anatoa miongozo namna tunavyopaswa kutoa bima kama alivyotoa miongozo Katika bima zote za magari, Viwanda na Mashine,tunatoa miongozo iliyotolewa na mamlaka ya bima
Aidha Amebainisha kuwa Tunaunga mkono Kwa serikali Kwa kutoa elimu Sasa bima inaweza kukufikia hata huko ulipo Kupitia chama chako Cha ushirika tunapitia huko Kwa mabenki au mawakala Wetu tuna mabranch 9 Kwa nchi nzima
Aidha NewTan Insurance ni jina jipya Kwa Sasa ambalo Kwa Mwanzo lilikuwa inaitwa UAP insurance Kwa mabadiliko hayo huduma Bado zitaendelea kuboreshwa
About The Author
Last modified: January 20, 2025