Visit Sponsor

Written by 12:47 pm KITAIFA Views: 6

DODOMA HAPATOSHI

Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI

-DODOMA

WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM), kikitarajiwa kuanza kwa Mkutano Mkuu Maalum kesho, hali ya hekaheka za wajumbe kutoka mikoa mbalimbali imeshika kasi jijini Dodoma.

Kutokana na hali hiyo ni wazi kwa siku ya jana Jiji la Dodoma lilikuwa na shangwe huku naba kubwa ya wajumbe kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Mtwara na Lindi waliwasili kwa kutumia treni ya kisasa ya SGR ambayo iliwabeba kuanzia jijini Dar es Salaam kuanzia saa 4 asubuhi ya jana na kuwasili Dodoma saa 8 mchana.

Mbali na wjaumbe pia miongoni mwa viongozi waliosafiri kwa na treni hiyo ni Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete kutoka kituo cha treni ya reli ya kisasa (SGR) Dar es Salaam, tayari kuelekea Jijini Dodoma kushiriki mkutano mkuu maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa utakaofanyika Januari 18 na 19, 2025.

Katika hilo Kundi la wajumbe 750 wa Mkutano Mkuu maalumu wa CCM Taifa liliondoka jana mkoani Dar es Salaam kuelekea Dodoma kwa kutumia usafiri wa treni ya SGR.

Katika hali ambayo ilivutiwa watu ni baadhi ya mabehewa ambayo walikuwa wamepanda wajumbe hao wakiongozwa na wenyeviti wa mikoa na maatibu ambao walikuwa wamepambwa na sare za kijani na nyeusi huku nyingi za CCM zikisikia na wengine kushangilia kwa kusema ‘Samia Mitano tena’ wakiashirikia kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuelekea Oktoba mwaka huu.

Baadi ya wajumbe ambao walizungumza na gazeti hili wakiwa katika Stesheni ya Samia Suluhu Hassan mjini Dodoma, alisema kuwa wamekuja mkoani hapa kwa jukumu la kuhakikisha wanakwenda kukiheshimisha chama kwa kupata Makamu Mwenyekiti bora na sahihi ambaye atakwenda kumsaidia kazi Rais Dkt Samia.

Akizungumza huku akipanda kwenye gari maalumu mmoja wa mjumbe wa Mkutano Mkuu kutoka Mkoa wa Lindi, aiyeitamulisha kwa jina la Juma Mipango, alisema kuwa katika mkoa wao wamejipanga kuhakikisha wanamuunga mkono Rais Saia hasa kutokana na kazi kubwa aliyoifanya kwenye ujenzi wa miradi mikubwa ya kimkakati katika maeneo mbalimbali nchini.

“Mimi nimekuja Dodoma kumsiliza Rais Samia akileta pendekezo la nani awe Makamu Mwenyekiti wetu, sisi ttaliunga mkono kwa sababu CCM tnataka kushinda uchaguzi na si muda wa maneno.

“Katika hili linapenda kusema pia kama kuna watu wana mipango ya kutaka kumkwamisha Rais Samia waandike maumivu, hatuko tayari kuona wamishaji wa chama wanapata nafasi ya kutupotezea muda,” alisema Mipango

Kwa upande wake Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Jawadu Mohammed alisema Mkutano Mkuu wa CCM Taifa utaibua fursa mbalimbali na kuchochea uchumi wa wakazi wa Dodoma wakiwemo waendesha pikipiki maarufu bodaboda.

“Sisi kama Mkoa wa Dodoma kwanza ni fursa kubwa sana kwa mkutano huu kwa sababu unakwenda kuchochea uchumi wa waendesha bodaboda ambao ni maafisa usafirishaji. Tayari tumeshazipata salamu za ongezeko la watu wengi wanaopanda bodaboda, ni kipato kinaingia,” alisema Jawadu

Licha ya hali hiyo alisema kuwa mkutano huo unakwenda kuongeza fursa kwa Mama Lishe, kwani wageni wengi wanaoshiriki mkutano huo watahitaji huduma kutoka kwao.

“Mkutano huu unakwenda kuongeza fursa kwa mama lishe wanaopika, ambapo tayari wameshatueleza. Na ukipita ukafanya utafiti hali ilivyobadilika, wingi wa wateja na wageni mbalimbali…hii yote ni fedha,” alisema Jawadu

CCM NA HOTELI 700

Kutokana na hali hiyo siku ya jana mji wa Dodoma kwa wageni ambao walikuwa wamekuja kwa lengo kuaka kuata hoteli hali ilikuwa tofauti kwa siku ya jana.

Hata hivyo chanzo kimoja utka ndani ya CCM kiliambia Wamachinga kuwa hoteli zaidi ya 700 zimechukuliwa na CCM kwa lengo la kuhudumia wajumbe kuanzia jana.

MGEJA ATOA NENO

Mwanasiasa mkongwe na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja, amewatakia heri wana-CCM katika mkutano mkuu wa kushika mikoba ya aliyekuwa Makamu Mwenyekiti, Abdulahman Kinana.



Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, amesema kuwa shauku kubwa ya wana-CCM ni kumpata Makamu Mwenyekiti atakayemsaidia mwenyekiti wa chama ambaye ni Rais Samia Suluhu Hassan.

“Nina imani kuwa atapatikana Makamu Mwenyekiti atakayemsaidia mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Samia kwani CCM ina hazina kubwa ya viongozi na wenye uwezo wa kuongoza katika nyanja mbalimbali,” alisema Mgeja.

Mgeja alisema kuwa shauku kubwa ya Watanzania ni kuona nafasi ya Makamu Mwenyekiti ambaye atarithi mikoba ya Kinana na kuweza kutimiza majukumu yake mapya kwa ushirikiano wa wana-CCM na pia kumsaidia na kumshauri mwenyekiti wa CCM.

“Tunaamini kuwa atakayepatikana atakuwa ni mwenye kumshauri mwenyekiti wa CCM Rais Samia katika kuleta mabadiliko ndani ya chama hivyo ni vyema sasa tukasubiri Mkutano Mkuu wa CCM unatarajiwa kufanyika Januari 18 hadi 19, 2025, jijini Dodoma,” alisema

Kabla ya Mkutano Mkuu, kikao cha Kamati Kuu kinafanyika leo ambacho kitatoa mapendekezo rasmi.



Awali Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla alisema mkutano huo wa CCM utaambatana na vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa, ambapo ajenda zitahusu kufanya uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, kupokea taarifa ya utekelezaji wa kazi za chama kwa kipindi cha mwaka 2022 hadi 2025, pamoja na taarifa ya utekelezaji wa Ilani kwa pande zote mbili, Bara na Zanzibar.

Kuhusu mchakato wa kumrithi Kinana, alisema mrithi wa nafasi hiyo anatarajiwa kupatikana baada ya Kamati Kuu kuwasilisha mapendekezo ya jina kwa halmashauri kuu kisha halmashauri kuu kuwasilisha jina hilo kwa wajumbe wa mkutano mkuu kwa ajili ya kupigiwa kura.

About The Author

(Visited 6 times, 1 visits today)

Last modified: January 20, 2025

Close