Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI
-DODOMA
WAKATI joto la kutaka kujua nani atarithi nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyokuwa inashikiliwa na Komredi Abdulrahman Kinana sasa ni wazi vikao vya mchakato vitaanza rasmi kesho.
Hatua hiyo inatokana na chama hicho tawala kuitisha Mkutano Mkuu Maalum ambao utakuwa na ajenga mahususi ikiwamo kujaza nafasi ya Makamu Mwenyekiti upande wa Bara pamoja na kupokea taarifa za Utekelezaji wa llani kwa Serikali ya Muungano na ile ya Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Katibu wa NEC, Itikadi na Mafunzo, Amos Makalla, ilieleza kuwa kesho Januri 17, 2025 kitafanyika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ambacho kitaongozwa na Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
“Aidha, kikao cha NEC kitatanguliwa na kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kutakachofanyika siku ya tarehe 17 Januari 2025, Dodoma
“Vikao hivyo ni sehemu ya maandaizi ya kuelekea Mkutano Mkuu Maalum utakaofanyika tarehe 18 a 19 Januari 2025, Dodoma,” alisema Makalla katika taarifa
Hata hivyo makada kadhaa wanatajwa huenda mmoja wapo akateuliwa na kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti ambao Abdallah Bulembo, Mizengo Pinda, Steven Wasira.
Bulembo amepata kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama cha Mpi ra wa Miguu Tanzania (FAT) sasa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), na pia kiongozi wa timu na vyama vya mpira wa miguu.
Hivyo CCM inayo hazina ya wanachama wake ambao wana sifa nyingi za uongozi ikiwamo hiyo ya ziada ambayo ni upenzi wa michezo.
Hivyo aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Abdulrahman Kinana, Mwenyekiti mpya awe Pinda, Bulembo, Wasira, Anne Makinda au mwingine.
Ni tunu au zawadi toka kwa Mungu ambayo hakuna anayeweza kutunyang’anya au kutuibia mpaka tutaka pokufa.
Hivyo, haitarajiwi nafasi ya Makamu Mwe nyekiti CCM kupewa mtu wa kujifunza au kufanya majaribio, inatakiwa mwe nye kipaji cha uongozi.
Si nafasi ya kujifunzia na kwa ukubwa na uko mavu wa CCM, itapendeza zaidi Makamu Mwenyekiti mpya akafanana na waliomtangulia.
Afanane na akina Mzee John Malecela, Mzee Pius Msekwa, Mzee Philip Mangula, na Komredi Abdulrahman Kinana katika kukabili siasa za ushin dani wa vyama vingi na kudhibiti makundi ndani ya CCM hasa kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Makamu wenyeviti niliowataja awali, kila mmoja na haiba yake, lakini wote wanafanana kwa uwezo, hekima na busara katika kushughulikia masuala ya siasa hasa ya chama tawala.
CCM wanahitaji Makamu Mwenyekiti msemaji, mwenye mvuto, ushawishi wa makundi na rika tofauti, mtu mkweli na asiyeyumbishwa kwa maslahi binafsi au ya kikundi.
Makamu Mwenyekiti mpya wa CCM ni lazima awe na mtaji binafsi wa kumuongezea kura mgombea urais wa CCM katika Uchaguzi Mkuu.
About The Author
Last modified: January 20, 2025