Visit Sponsor

Written by 7:44 pm KITAIFA Views: 10

RAIS SAMIA AREKEBISHA BARAZA LA MAWAZIRI,BASHUNGWA AKABIDHIWA JESHI LA POLISI

Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI

-DAR ES SALAAM

RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan amelifumua Baraza lake lake la Mawaziri kwa kufanya mabadiliko madogo na kuwateua viongozi mbalimbali ambapo huku Profesa  Palamagamba Kabudi amemteua kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, akitokea Wizara ya Katiba na Sheria.

Mbali naye huku Innocent Bashungwa akiteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, akichukua nafasi ya Hamadi Masauni, awali Bashungwa alikuwa akihudumu kama Waziri wa Ujenzi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyolewa jana Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu, Balozi Moses Kusiluka na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Sharifa Nyanga, ilieleza kuwa katika mabadiliko hayo  Rais Samia, amemuhamisha Dkt. Damas Ndumbaro kwenda kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, ambap awali alikuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo ambapo Wizara hiyo kwa sasa itaomgozwa na Prof. Palamagamba Kabudi.

Mbali nae katika nabadiliko hayo yamemgusa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira, Dkt. Ashatu Kijaji ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi huku aliyekuwa Waziri wa wizara hiyo, Abdallah Ulega akipelekwa kuwa Waziri wa Ujenzi.

Mbali na hilo Jerry Silaa, ameteuliwa kuwa Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari akiondolewa jukumu la Sekta ya Habari ambalo sasa limerudi kwenye Wizara ya Michezo kama ilivyokuwa awali.

Makatibu wakuu, manaibu

Katika panga pangua hiyo ya Rais Samia, amefanya uteuzi wa Gerson Msigwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali.

Msigwa licha ya kuwa Katibu Mkuu ameongezewa jukumu la Usemaji Mkuu wa Serikali akichukua nafasi ya Thobias Makoba aliyekuwa Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye ameteuliwa kuwa Balozi na atapangiwa kituo cha kazi.

“Dkt.James Kilabuko ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu). Dkt. Stephen Nindi ameteuliwa kuwa ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Ushirika na Umwagiliaji, huku Dkt Suleiman Serera amehamishwa kwenda kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara huku Dkt John Smbachawane ambaye atapangiwa kituo cha kazi

“Profesa Mohammed Janabi, ameteliwa kuwa Mashauri wa Rais Masuala ya Afya na Tiba aidha pamoja na hilo Prof Janabi ataendelea kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,” ilieleza taarifa hiyo ya Ikulu

Mabalozi

Pamoja na hayo Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya viongozi mbalimbali ambapo amewateuwa Mobhare Matinyi na Thobias Makoba kuwa mabalozi, ambao watapangiwa vituo vya kazi hapo baadae.

Pia Rais Samia amemteua Kamishna wa Polisi Zanzibar, CP Hamad Khamis Hamad pamoja na CP Suzan Kaganda ambao wameteuliwa kuwa mabalozi na watapangiwa kituo cha kazi.

Viongozi wote walioteuliwawataapishwa kesho Desemba 10, Ikulu Ndogo, Tunguu Zanzibar saa tano asubuhi.

About The Author

(Visited 10 times, 1 visits today)

Last modified: December 12, 2024

Close