Visit Sponsor

Written by 7:39 pm KITAIFA Views: 7

RAIS SAMIA AFICHUA SIRI UKUBWA WA PROF.JANAB

Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI



-ZANZIBAR

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa Mohamed Janabi kujiandaa kugombea nafasi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, Dkt Faustine Ndugulile.

Dkt Ndugulile ambaye pia alikuwa Mbunge wa Kigamboni, alifariki dunia Novemba 27, mwaka huu ikiwa ni miezi kadhaa baada ya kushinda nafasi hiyo.

Akizungumza baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali jana Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar, Rais Samia amesema wamepitia wasifu zaidi ya tano kubaini kwamba Profesa Janabi ana sifa ya kurithi mikoba hiyo.

“Naomba nifichue siri hapa, tumepitia zaidi ya CV tano na tukaona Profesa Janabi anafaa kuchukua nafasi ya Dkt. Ndugulile. Hivyo, tunakundaa kwenda kugombea nafasi hiyo muda utakapofikia. Ujiandae,” alisema Rais Samia.

Akizungumzia uteuzi wa viongozi kwenye nafasi mbalimbali, Rais Samia alisema kuwa ni jambo la kawaida katika kuimarisha utendaji wa Serikali.

“Ninawapongeza mlioteuliwa, mliobadilishwa tu nafasi zenu hakuna uteuzi mpya isipokuwa labda kwa upande wa mabalozi labda, lakini wengi mmebadilishwa tu nafasi zenu na shughuli hii ya ubadilishanaji ni kwa ajili tu ya kuongeza ufanisi ndani ya serikali.

“Ombi langu kwenu mlioapa na mnaokwenda kwenye maeneo mapya, ninajua mlijijenga vizuri kwenye wizara zenu mlizokuwepo na wengine mmebadilishwa kwenda wizara zingine, lakini serikali ni ileile, sheria ni zilezile, majukumu tu yanabadilika, ninaomba mkawatumie ipasavyo mnaowakuta kule, Makatibu Wakuu na wataalamu mnaowakuta kule,” alisema Rais Samia.

Kutokana na hali hiyo aliwapongeza mawaziri wapya, ambapo alimpongeza Waziri mpya wa Muungano na Mazingira, Hamad Masauni ambaye alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani kuwa alifanya kazi nzuri.



Aidha, alimtaka akafanye vizuri katika wizara yake mpya huku akimuambia amemrudisha karibu na jimbo lake la Kikwajuni.

“Masauni twende ukaimarishe muungano wetu, ni wasifu (CV) mwingine kwako, lakini ndiyo sababu ya kurudi Kikwajuni (Jimbo la mbunge Hamad Masauni ambaye ameapisha kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira; awali alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi) sasa ukae muda mrefu pale kwasababu ninasikia watu wanalimendea jimbo.

“Sasa wewe katika kuimarisha muungano muda wote utakuwepo pale. Umefanya kazi nzuri Wizara ya Mambo ya Ndani sasa nenda kaimarishe muungano, nenda kwenye mazingira, lakini hiki ni kipindi kizuri hiki cha kukaa Kikwajuni na mambo mengine tutanong’ona kwa siri, ya kufanya ukiwa huko,” alisema Samia.

Pamoja na hali hiyo alimsisitiza Waziri mpya wa Habari Michezo Sanaa na Utamaduni Profesa Palamagamba Kabudi kuikamata vizuri sekta ya habari kwani alipitia wasifu wake (CV) nakuona kumbe ni mwanahabari hivyo matatizo ya wanahabari anayajua vyema akashughulike nayo.



Kuhusu Michezo, Sanaa na Utamaduni Rais Samia aliema atakuwa akimtumia vyema kijana Hamis Mwijuma ambaye ni Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Rais Samia Suluhu Hassan alitaja sababu za kuitoa sekta ya habari katika Wizara ya Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na kuipeleka kwenye Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Miongoni mwa sababu ni kuipa nguvu teknolojia ya habari ambayo amesema kama ilisahaulika na nguvu kubwa iliwekwa kwenye habari.

“Dada Aisha nakuondosha hapa nakuweka hapa, lakini ndio kazi za serikali nimekupeleka Mifugo na Uvuvi sasa hiyo high heels ikavuke zile jeans ulikoficha ukafukue,” hayo ni maneno ya Rais Samia Suluhu Hassan akizumngumzia Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dkt. Ashantu Kijaji.

MAKAMU WA RAIS

Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amewataka viongozi walioteuliwa kuheshimu mawazo ya wataalamu katika ofisi zao na wasiwe wababe.



Dkt. Mpango alisema hayo Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar alipokuwa akitoa salamu za pongezi kwa wateule hao kabla ya kumkaribisha Rais Samia Suluhu Hassan kutoa hotuba.

“Nawasihi mkafanye kazi yenu na mkashirikiane na wenzenu mtakaowakuta, tukacheze kama timu ya ushindi..mkaheshimu mawazo ya wataalamu mtakaowakuta kwenye ofisi zenu,”alisema.

About The Author

(Visited 7 times, 1 visits today)

Last modified: December 12, 2024

Close