Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI
Dar es Salaam
Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania Jaji Joseph Sinde Warioba alizungumza na wanahabari siku ya Jumatano Desemba 04, 2024 mkoani Dar es Salaam kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 27, 2024.
Jaji Warioba awataka vyama vya upinzani kuacha malalamiko dhidi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwani ni dhahili kwamba hawakuwa na mpango madhubuti wa kuingia katika chaguzi hizo.
โNilimuuliza kiongozi mmoja wa upinzani. Je, kweli mnategemea nini? Akaniambia walikuwa wamefanya utafiti. Matokeo yake tuliyoonyeshwa tukijitahidi sana upinzani kwenye uchaguzi wowote unaokuja hatutazidi asilimia 25. Wakijua kwamba wao kwa wakati huu hawana uwezo wa kuweza kutoa ushindani mkubwa,โWaziri Mkuu mstaafu Jaji Sinde Warioba.
About The Author
Last modified: December 6, 2024