Visit Sponsor

Written by 4:23 am KITAIFA Views: 5

WARIOBA AWATAKA POLISI WASIGUSE SIASA

Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI

Jeshi la Polisi limetakiwa kutojihusisha katika masuala ya siasa badala yake lijikite kufanya kazi yake ya kulinda usalama wa raia na mali zao.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Warioba wakati akitoa tathimini yake ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa hii leo.

Amesema kuwa jeshi litakapoingia kwenye siasa litaleta mgawanyiko mkubwa kwa wananchi.


“Jeshi la Polisi kazi yake ni kulinda usalama wa wananchi halipaswi kujikita wala kujiingiza kwenye siasa, hali itakayopelekea kuwagawa wananchi, “

“Polisi wamekuwa wakitoa matamko ya kisiasa jambo ambalo sio sahihi wakati wanapaswa kulinda Usalama katika jamii na linatakiwa kufanyakazi zake za kawaida la sivyo watajenga uadui na wananchi,”amesema Jaji Warioba

Pia ameongeza kuwa Rais achukue hatua matatizo yametokana na awamu ya tano japo kuwa alipoingia aliadithia hayo matatizo anapaswa kuzidi kuyafanyia kazi.

“Japo alipoingia tumeona Baadhi ya mambo aliweza kuondoka masharti kwa vyombo vya habari na kuwa huru na kuhusisha vyama vya siasa ambapo kafanyakazi nzuri.

“Vyama vya siasa wanatakiwa kuangalia maslai ya raia kuachana na chuki, uadui viangalie maslai ya Taifa na sio maslai ya chama vyao.

Yaliotokea kwenye uchaguzi amewaomba viongozi wa Chama cha Mapinduzi wanatakiwa wakae na viongozi waliopita na wenyeviti wa vyama waliopita pamoja na Marais waliopita kama kina (Malechela, Mangula) watawashauri jinsi ya kuendeshea uchaguzi.

Ameongeza kuwa Hakuna kitu cha msingi  kama amani na mshikamano tatizo hili linatokana na Serikali inatakiwa kuchukua hatua kuepuka matatizo haya yasijitokeze.

Aidha ameupongeza utendaji kazi wa Rais Magufuli  kwa kuwa na maamuzi magumu kwa kumbukumbu ya vitu mfano kuamisha makao makuu kwenda Dodoma, Relief mpya na kwenye miundombinu amefanikisha pakubwa.

About The Author

(Visited 5 times, 1 visits today)

Last modified: December 5, 2024

Close