Visit Sponsor

Written by 2:55 pm KITAIFA Views: 8

NAIBU WAZIRI SANGU AWATAKA WANACHI KUICHAGUA CCM, AMTAJA RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN




Na Mwandishi Wetu – Rukwa

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma a Utawala Bora ambaye pia  ni Mbunge wa Kwela, Mhe.Deus Sangu  amewataka wananchi wasisahau maendeleo wanayoyaona katika Jimbo la hilo  ni kutokana  na jitihada za  Rais Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan   kupitia Chama Cha Mapinduzi.

Ameyasema hayo  leo wakati akizungumza kwenye mkutano wa Kampeni za Serikali za Mitaa uliofanyika katika Kjiji cha Ilemba,  Kata ya Kalambanzite katika Jimbo la Kwela Mkoani  Rukwa.



Amefafanua kuwa ndani ya kipindi cha miaka mitatu ya Rais Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Kata ya Kalambanzite imeimarika katika sekta ya afya, elimu, barabara, maji pamoja na umeme.

Amewataka wananchi hao kujitokeza ifikapo Novemba 27 mwaka huu  ili  kuchagua viongozi wenye maono na mwelekeo wa kuwaunganisha kuanzia ngazi ya shina hadi Taifa ambao ni Wagombea kupitia CCM.



” Chagueni viongozi ambao wana uelewa wa matatizo na kujua namna ya kutatua changamoto zinazowakabili wananchi pasipo kujali rangi, kabila au eneo” amesema Mhe.Sangu

Mhe.Sangu amewaeleza Wanachi wa Kata hiyo ya Kalambanzite  kuwa wana kila sababu ya  kuchagua  Chama chenye Sera zinazotekelezeka ambacho ni Chama Cha Mapinduzi na kuachana na vyama  vingine ambavyo sera zao   zimelenga kuhubiri chuki na utengano.



“ Nimekuja kuwaomba mtuunge mkono kwa kupiga kura na kuchukua vijiji na vitongoji vyote” ameomba Mhe.Sangu

Naye Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa  wa Rukwa, Patrick Maufi amewashukuru wagombea waliopitishwa na kusema hadi sasa CCM imesimamisha wagombea bila kupingwa  katika ngazi mbalimbali katika uchaguzi huu.

Hata hivyo Mjumbe huyo amewataka Wananchi wakapige kura ya ndiyo kwa  baadhi ya wagombea waliopita bila kupingwa.

About The Author

(Visited 8 times, 1 visits today)

Last modified: November 23, 2024

Close