Na. Lusungu Helela-Katavi
Serikali imewataka Watumishi wa Umma nchini kuwasilisha changamoto zao za kiutumishi wakati wowote na mahali popote ili ziweze kufanyiwa kazi lengo likiwa ni kumsaidia Mtumishi kutatuliwa changamoto zake pasipo kulazimika kusafiri kuja jijini Dodoma
Ametaja mifumo hiyo ya kidijitari ikiwemo e-Mrejesho, Sema na Waziri wa Utumishi pamoja na njia ya kupiga simu ambapo hadi sasa njia hizo zimesaidia kuleta mageuzi makubwa katika uboreshaji wa utoaji wa huduma bora kwa wananchi wakiwemo Watumishi wa Umma
Mhe.Sangu ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, Mkoani Katavi, ikiwa ni muendelezo wa kliniki ya kimkakati ya kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili Watumishi hao.
Akifafanua mfumo wa kidijitari wa “Sema na Waziri wa Utumishi” Mhe.Sangu amesema mfumo huo unamusaidia Mtumishi wa Umma kuwasiliana ana kwa ana Waziri mwenye dhamana na Utumishi wa Umma nchini
Katika kikao hicho Naibu Waziri ameambatana na timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kushirikiana na Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kwa ajili ya kuzifanyia kazi chagamoto hizo za Watumishi wa Umma wakiwemo walimu katika Halmashauri hiyo.
Amesema moja ya jukumu la Serikali ni kuhakikisha watumishi wa umma wanatatuliwa changamoto wakiwa kwenye vituo vyao kazi ili kuwafanya wananchi waendelee kupata huduma.
Amesema Watumishi wa umma kama ilivyo kwa wananchi wa kawaida wana haki ya kuhoji na kutoa malalamiko yao pindi wanapoona madai au stahiki zao hazitimizwi
Amesisitiza kuwa mifumo hiyo inachochea na kuihimiza Serikali kuwajibika kwa wananchi moja kwa moja na kumuwezesha hata mtu wa chini kabisa kuwasiliana moja kwa moja na mamlaka za juu
Kufuatia hatua hiyo, Mhe.Sangu amesema Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imekuwa ikipokea malalamiko pamoja na madai mbalimbali ya watumishi na kufanyiwa kazi kwa haraka.
Akizungumzia mafanikio ya Mifumo hiyo ukiwemo mfumo wa e-Mrejesho, Mhe.Sangu amesema mfumo huo unampa fursa mwananchi kutuma na kupokea malalamiko pamoja na maulizo kwa Serikali, kutokana na umadhubuti wake umeweza kupata tuzo ya kimataifa.
Hivi karibuni Tanzania ilipewa tuzo ya Kimataifa ya ubunifu wa mfumo ya kidijitali wa Mrejesho (e-Mrejesho)
nchini Korea Kusini na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) wakati wa Mkutano wa Umoja wa Jukwaa la Umoja wa Mataifa la Tuzo za Utumishi wa Umma (2024 UN Public Service Awards (UNPSF).
About The Author
Last modified: November 19, 2024