Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan Amesema Jumla ya watu 84 wameokolewa na kufikishwa hospital Kwa ajili ya kupatiwa matibabu na kati ya hao majeruhi 26 Bado wanaendelea na matibabu na watu 13 wamepoteza maisha Katika tukio hilo.
Amesema serikali itabeba Gharama za matibabu Kwa wote waliojeruhiwa na kuhakikisha Kwa waliofariki wanasitiriwa ipasavyo
Aidha Ametoa pole Kwa ndugu na jamaa na marafiki walioguswa na tukio hilo
Amewaomba watanzania wote waweke kwenye maombi Kwa wale walioathirika na tukio hili na kuwaombea pumziko ya amani Kwa wezetu waliotangulia mbele za haki
Hata Hivyo Amesema Serikali itaendelea kutoa taarifa Zaidi Kuhusu zoezi la ukoaji na uokozi Hadi zoezi hili litakalo kamilika,Hadi Sasa sababu za kiutaalamu Kwa jengo hilo kuporomoka Bado hazijachunguzwa na kubainishwa kwani kipaumbele chao ni kwanza ilikuwa ni kuwaokoa wenzetu waliokuwa ndani ya jengo hilo
“Navipongeza na kuvishukuru vyombo vyote vya usalama Ambapo Bado wanaendelea na zoezi hilo la ukoaji wa ndugu zetu waliokubwa na kazia hii,
Vilevile ninashukuru mashirika binafsi na wananchi waliojitolea na waliojitoa na waliotoa ushirikiano wa zoezi hilo.Pia ninawashukuru madaktari wanaoendelea kuwahudumia wananchi”
Vilevile Amemtaka waziri mkuu aongoze timu Kwa wakaguzi majengo waendelee na zoezi la kukagua eneo lote la kariakoo na kupata taarifa kamili ya hali ya majengo ya kariakoo ilivyo
Kwa upande mwingine jeshi la polisi linatakiwa kupata taarifa kamili Kwa mmiliki wa jengo lililoporomoka jinsi ya ujenzi uliokuwa ukifanyika
Wananchi serikali inahakikisha munapata ushirikiano wake Kwa ziaa mwanzo wa zoezi hili Hadi mwisho na kwamba taarifa za uchunguzi zitakapo patikana basi taarifa hizi zitaekwa wazi Kwa wananchi wote na hatua zitawekwa wazi Kwa wananchi wote na hatua zitakazochukuliqa zitawlwza Kwa kina.
About The Author
Last modified: November 18, 2024