Visit Sponsor

Written by 6:46 pm KITAIFA Views: 3

RV CHALAMILA AKANUSHA SHULE YA MSINGI NATIONAL HOUSING KUUZWA

Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI



-Asema jamii ipuuze uvumi unaosambaa wa kuuzwa kwa shule hiyo.

-Akiri dhamira ya Serikali kufanya maboresho makubwa ya ukarabati shule hiyo.

-Aagiza ukarabati ukianza ambao utahusisha pia ujenzi wa majengo ya Ghorofa usiathiri wanafunzi kuondoka

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Novemba 13, 2024 amefika katika shule ya msingi National Housing wilaya ya Ubungo Jijini humo na kukanusha uvumi uliokuwa ukisambaa kupitia mitandao ya kijamii kuwa shule hiyo inayomilikiwa na serikali imeuzwa.

RC Chalamila ameitaka jamii kupuuza uvumi huo ambao sio kweli shule ni mali ya serikali na itaendelea kuwepo siku zote hivyo jamii na wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo waondoe shaka shule itaendelea kubaki hapo hapo

“Hakuna mwanafunzi ataondolewa kutoka Shule ya Msingi National Housing kwenda shule ya msingi Ubungo Plaza” Alisisitiza RC Chalamila.

Aidha RC Chalamila amefafanua dhamira ya Serikali kuboresha miundominu ya shule hiyo ikiwemo ukarabati na kwa siku za mbeleni ujenzi wa madarasa ya ghorofa kutokana na uhaba wa maeneo na hiyo ni sera ya Mkoa ili kuwa na matumizi bora ya Ardhi vilevile ameagiza shughuli hizo zitakapotekelezwa zisiathiri wanafunzi kuondoka katika shule hiyo.

Sanjari na hilo RC Chalamila alipata wasaa wa kuongea na wanafunzi na kuwataka kusoma kwa bidii, shule ipo haiwezi kuuzwa hivyo waondoe shaka.

Ifahamike kuwa shule ya msingi National Housing iliyoko nyuma ya Jengo la Ubungo Plaza inaendelea bado kutoa huduma  wanafunzi sio chini ya 600 wanasoma katika shule hiyo.

About The Author

(Visited 3 times, 1 visits today)

Last modified: November 13, 2024

Close