Visit Sponsor

Written by 6:08 am KITAIFA Views: 5

DK CHANG’A ATUNUKU VYETI WANAFUNZI WA SHAHADA YA UZAMIVU KATIKA SAYANSI YA MABADILIKO YA TABIANCHI,MONACO

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

Monaco, 7 Novemba 2024
Dk.Ladislaus Chang’a, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (Intergovernmental Panel on Climate Change-IPCC), amealikwa kuhudhuria na kutunuku Tuzo wakati wa Sherehe za 17 za Tuzo ya Kimataifa ya Afya ya Mfuko wa Mwana Mfalme Albert II wa Monaco, “17th Planetary Health Awards Ceremony of the Prince Albert II of Monaco Foundation”, ambapo wanafunzi wa Shahada ya Uzamivu waliofaidika na mfuko huu wametunukiwa tuzo kwa kazi zao za utafiti ikiwa ni sehemu ya ushirikiano ulioanzishwa kati ya mfuko huo na IPCC.

Tukio hilo lenye hadhi kubwa katika tasnia ya sayansi ya mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi Duniani lilifanyika siku ya Alhamisi, 7 Novemba, 2024 katika ukumbi wa Opera Monte-Carlo, huko Monaco na kuongozwa na Mfalme Albert wa II wa Monaco. Aidha, Dkt. Chang’a amekasimiwa pia na IPCC jukumu la kuwa Mwenyekiti wa Mfuko wa Ufadhili wa Masomo wa IPCC (IPCC Scholarship Fund).

Hafla hii ya kutunuku vyeti aliyoshiriki Dkt. Chang’a ni heshma kwa Tanzania na Afrika, na imeendelea kuitangaza nchi yetu Kimataifa.

About The Author

(Visited 5 times, 1 visits today)

Last modified: November 9, 2024

Close