Visit Sponsor

Written by 5:30 pm KITAIFA Views: 3

MCHENGERWA RAIS SAMIA KUFANYA UBORESHAJI MKUBWA KATIKA JIJI LA MWANZA

Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Seikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa amesema kazi kubwa ya ujenzi wa miundimbinu ikiwemo ya barabara katika Jiji la Mwanza ni utekelezaji wa dhamira ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kufanya uboreshaji mkubwa katika jiji hilo.


Amesema Rais Samia Samia ametoa zaidi ya sh. bilioni 24 kwa ujenzi wa badabara za lami katika jiji hilo na kuupongeza Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) kwa usimamizi mzuri huku akiwapa angalizo wakarasi waliopewa kazi ya ujenzi kuwa hakutaongezwa hata siku moja baada ya muda wa makubaliano kukamilika.


Mchengerwa ameyasema hayo leo Oktoba 16, 2024 katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza aliposhuhudia utiaji saini mikata…
“Leo tunashuhudia wilaya zetu hizi mbili Nyamagana na Manispaa ya Ilemela wanakwenda kupata faida kubwa ya maono ya Rais wetu Dk. Samia, fikra za kuboresha maeneo yetu ni fikra za Rais Samia.


“Utekelezaji huu tunaokwenda kuufanya leo si kwa bahati mbaya, ni kwa sababu Rais wetu Dk. Samia ameingia kwenye mioyo ya Watanzania wa kawaida kabisa, amekusudia kuboresha vijiji, kuwa miji vitongoji kuwa vijiji na miji kuwa majiji.


“Fikra hizi ni maono ya Baba wa Taifa (Hayati Mwalimu Julus Nyerere) ambayo yanatekelezwa leo na Rais Dk. Samia, hakuwa kiongozi mwingine yeyote isipokuwa Rais Dk. Samia, anayafanya haya kwa mapenzi ya dhati ya Watanzania walioko katika maeneo mbalimbali,” alisema.


Kwa mujibu wa Waziri Mchengerwa, takwimu zinaonyesha namna Rais Dk. Samia amekusudia kuleta mapinduzi makubwa kwa kuboresha miji, majiji na halmashauri za wilaya.
Alisema analolifanya Rais Samia anakusudia kuingia katika maisha ya Watanzania wa kawaida ambao wanashuhudia utekelezwaji wa miradi hiyo.


“Miradi hii si bahati mbaya kama ambavyo nimetangulia kusema, miradi hii si starehe, miradi hii ni mafanikio makubwa ambayo wananchi wa Mwanza mnakwenda kuyapata, utekelezaji wa miradi hii unakwenda kumgusa kila Mtanzania mwenye kipato na asiye na kipato.


“Wapo ambao watanufaika na fedha zinazotekelewa katika miradi hii, wapo watakaotumia sehemu ya miradi hii, wako watakaotumia barabara, kama ulikuwa unatembea kwa saa mbili sasa watatumia nusu saa, kama walikuwa wanapata shida kwenda kununua mazao na kuyafikia masoko sasa kila Mtanzania anayeishi Jiji la Mwanza atanufaika kwa kununu mazao.


“Mtendaji wa TARURA mchapakazi Sefu amesema hapa kuhusu miradi inayoendelea Mwanza, miradi hii aliifikiria Rais Samia akasema anatamani iende kwanza Mwanza, hakufikiria kwingine kokote alianza kufiria Mwanza,” alisema.


Alipongeza kazi kubwa inayoendelea kufanyika Mwanza hususan katika wilaya ya Ilemela ambako miradi mbalimbali inaendelea kutekelezwa, huku pia kukiwa na baadhi ya mikata imetiwa saini na sasa inasubiriwa utekelezaji.


“Nina taarifa kwamba mradi wa ujenzi wa Barabara ya Buswelu-Nyamanoke unaendelea vizuri, mradi wa Buswelu-Cocacola unaendelea vizuri,” alisema.


Kwa mujibu wa Mchengerwa, matarajio ya miradi inayoendelea zikiwa ndoto za Rais Samia kuwafikiria Watanzania wa Ilemela katika maeneo mbalimbali vijijini na mijini ni fursa muhimu ya maendeleo.

MAELEKEZO MAHUSUSI
“Nichukue fursa hii kutoa maelekezo, kiwango cha fedha katika mradi huu unaoendelea ni zaidi ya sh. bilioni 22.7.
“Ninawaelekeza wakandarasi wanaotekeleza mradi huu makubaliano mwisho ni mwezi wa pili mwakani, hakutakuwa na nyongeza hata siku moja.
“Nimpongeze mbunge wa Nyamagana jambo hili alikuwa analipigania kila siku bungeni, mbunge anafanya kazi nzuri, ujenzi wa barabara ya lami kilometa zaidi ya 14 unaoendelea hapa Nyamagana, kutoka Igoma kwenda Buhongwa natambua kwamba mkandarasi yupo zaidi ya asilimia 60 ya utekelezaji, kiwango cha fedha ambazo Rais Samia ameleta ni zaidi ya sh. bilioni 24.


“Maelekezo yangu kwa viongozi ni kusimamia miradi hii, maelekezo yangu kwa wakandarasi hakutakuwa na nyongeza hata siku moja,” alisema.


Pia, aliwasihi madiwani wa Nyamagana na Ilemela kuendelea kufanya kazi kubwa ya kusogeza maendeleo kuhakikisha yanawafikia wananchi na kwamba, mipango ya maendeleo ianzie katika mabaraza ya madiwani.


Alisema anatambua kuwa wakurugenzi wamekuwa wakiwasikiliza madiwani wanapowaendea kuwaeleza kwamba wanakusudia kusogeza huduma za kijamii kwa wananchi.


“Niwaombe madiwani endeleeni kuwafikiria wananchi, endeleeni kuwafikiria wana Mwanza mkawaguse maisha yao. Kwa sababu Rais Dk. Samia anawategemea ninyi madiwani mkiwa wawakilishi wa karibu wa wananchi, ninyi ndio wawakilishi wa wananchi kule chini moja kwa moja,” alieleza.


Awali akizungumza katika hafla hiyo iliyoshuhudiwa na mamia ya wananchi wa Jiji la Mwanza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda, alisema serikali mkoani humo itaendelea kuisimamia kwa karibu miradu hiyo na mingine inayotekelezwa lengo lake ni kuwarahisishia wananchi upatikanaji wa huduma.


Pia, aliwapongeza wananchi wa Mwanza kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki sherehe za uzimaji mwenge zilizofanyika jijini humo Okroba 14, mwaka huu ambapo mgeni Rasmi alikuwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

About The Author

(Visited 3 times, 1 visits today)

Last modified: October 16, 2024

Close