Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI
RAIS Samia Suluhu Hassan amesema hadi sasa sekta ya madini ndiyo sekta inayoongoza kwa kuliingizia taifa la Tanzania fedha nyingi za kigeni ambapo mwaka 2023 sekta hiyo iliingiza takribani asilimia 56 ya fedha zote za kigeni zilizoingia nchini.
Ameyasema hayo jana mkoani Geita wakati wa Kilele cha maonesho ya Saba ya Teknolojia na Uwekezaji katika sekta ya Madini uwaja wa EPZA,alisema Serikali inatoa uzito mkubwa kwa sekta hiyo ya madini kwa kutambua nafasi ya sekta hiyo katika kubadili hali ya wananchi wake hususan wachimbaji wadogo na pia katika kukuza uchumi na kuliingizia taifa fedha za kigeni.
Alisema Serikali imekuw ikitoa kipaumbele katika sekta hiyo na kufatilia kwa ukaribu ni msingi wake wa kuona namna inavyoingiza fedha nyingi katika mfuko wa Serikali.
Rais Samia alisema katika mwaka wa fedha 2023/24,Serikali imeongeza bajeti katika wizara hiyo kutoka sh.Bil 89 kwa mwaka wa fedha 2022/23 hadi kufikia Bil. 231 kwa mwaka 2024/25.
Alisema ongezeko hilo la bajeti limelenga kuongeza ufanisi katika sekta hiyo ikiwa ni pamoja na kuimarisha mifumo ya ukusanyaji wa mapato,kuijengea uwezo taasisi ya jiolojia na utafiti wa madini ilikuweza kufanya utafiti wa kina na uwazi wa madini.
”Kama mnavyojua ndugu zangu madini tunayouza sasa maeneo yote yanayochimbwa sasa ni asilimia 16 tu ya nchi yetu ndio imefanyiwa utafiti,hivyo tunajipanga kununua helicopta na vifaa vyake ambavyo vitatusaidia kufanya utafiti nchi nzima na utafiti huo utuambia mkoa gani unamadini gani gani na kiasi gani,hapo tutakuwa tumejipanga vizuri,”alisema na kuongeza
”Tunawekeza fedha nyingi ili kufanya utafiti na tuwe na takwimu nzuri na zenye uhakika katika rasilimali hiyo ya madini,”alisema.
Alisema uwekezaji huo wa serikali utaleta matokeo yaliyokusudiwa ambapo tayari wameona muelekeo mzuri wa uwekezaji unaofanywa wa sekta hiyo.
Rais Samia alisema tayari wameona pato la taifa limeongezeka kwa upande wa sekta hiyo, kwa mfano mwaka 2023 katika pato la taifa mchango wa sekta ya madini ilikuwa asilimia 9 kutoka asilimia 7.2 mwaka 2021 lengo walilotoa kufikia asilimia 10 ifikapo mwakani 2025.
”Ongezeko hili la pato la taifa ni kutokana na kuweka mazingira mazuri ya ufanywaji wa shughuli za madini na upatikanaji wa teknolojia za kisasa ambapo serikali imefanya uwekezaji mkubwa kupitia stamico wameweza kununua mitambo 15 ya uchorongaji miamba ambapo mitambo mitano imefika nchini na 10 ipo njiani inakuja,”alisema.
Aidha alisema ujio wa mitambo hiyo itasaidia wachimbaji wadogo kupata taarifa za uhakika katika maeneo yao ya uchimbaji na kuwaepusha na hasara,pia mitambo hiyo 10 itakapofika itatawanywa katika maeneo yote ya uchimbaji.
Rais Samia alisema amemtaka waziri kutenga mitambo miwili kwa wachimbaji vijana na mtambo mmoja kwaajili ya wachimbaji wanawake na namna hali itapozidi huko mbele wataona namna ya kuongeza mitambo hiyo.
Alisema pamoja na hayo serikali imetenga Bilioni 250 kama dhamana ya mikopo kuwawezesha wanunuaji wa dhahabu,madini kuweza kukopa na kufanya kazi yao vizuri hivyo hivyo Benki ya Tanznia imeweka trilioni 1 kwaajili ya ununuaji wa dhahabu.
Alisema Serikali imesogeza huduma ya masoko kila mkoa na kuweka vituo vya kununulia madini katika maeneo yanayochimbwa ambapo hadi sasa kuna masoko 44 mikoa yote na vituo 113 na kuwepo kwa mzunguko mzuri wa ununuaji wa madini.
Alisema kwa mwaka 2023/24 madini yenye thamani ya trioni 2 yaliuzwa kupitia masoko ya madini na kuiwezesha serikali kukusanya kiasi cha bilioni 180 kutokana na masoko hayo mbali na mapato mengine yanayokusanywa na wizara.
Rais Samia alisema kabla ya kuja katika mkutano huo amefika katika soko la dhahabu la geita na kuona shughuli inayofanyika hapo,mpangilio mzuri na kuona wachimbaji wadogo walivyorahisishiwa kazi.
About The Author
Last modified: October 14, 2024