Visit Sponsor

Written by 3:28 pm KITAIFA Views: 40

TMDA YATADHARISHA WAFUGAJI WANAOTUMIA ARV KUNENEPESHA MIFUGO YAO

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM MWANAHABARI

Mamlaka ya dawa na Vifaa Tiba TMDA imesema kwamba imepata taarifa juu ya uwepo wa baadhi ya wafugaji wanaotumia vibaya dawa za kufubaza makali ya virusi vya ukimwi (ARV’S) Ili kunenepesha mifugo Yao.

Taarifa iliyotolewa Kwa vyombo vya habari na mkurugenzi mkuu wa TMDA Adam Fimbo amesema mamlaka hiyo inakemea matumizi hayo kwani yanamadhara makubwa Kwa Afya ya jamii.

Amesema kuwa dawa hizo zinatakiwa zitumike Kwa ajili ya kufubaza makali ya virusi vya ukimwi Kwa binadamu baada ya mgonjwa kushauriwa na daktari,na hivyo matumizi yake Katika kulisha mifugo kunahatarisha Afya ya jamii.

“TMDA inaelekeza wafugaji wote wanaofanya hivyo kuacha mara Moja.Aidha kuanzia Sasa TMDA imeanza uchunguzi wa kina Katika mashamba mbalimbali ya mifugo Ili kubaini wanaojihusisha na matumizi holela ya dawa na atakaebainika kufanya hivyo.atachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kuharibiwa Kwa mifugo yake kwani itakuwa mazao ya mifugo husika haifai tena Kwa matumizi ya binadamu”.Imesema taarifa hiyo

About The Author

(Visited 40 times, 2 visits today)

Last modified: September 22, 2024

Close