Visit Sponsor

Written by 7:53 am KITAIFA Views: 29

KAPINGA AFUNGUA KIKAO KAZI TPDC

Na Mwandishi Wetu MWANAHABARI



Awataka kuyapa kipaumbele masuala ya wafanyakazi.

Ataka changamoto ya wafanyakazi kukaimu muda mrefu kufanyiwa kazi

Naibu Waziri Nishati,  Mhe. Judith Kapinga leo Septemba 17, 2024 amefungua kikao kazi cha Menejimenti ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Jijini Mwanza.

Lengo la kikao hicho ni kujitathmini, kujipanga na kukumbushana masuala mbalimbali ya Taasisi, ikiwemo maelekezo mbalimbali ya Serikali ya uendeshaji wa kampuni.



Amewasisitize na kuwakumbusha umuhimu wa kufanya kazi kwa umoja, ubunifu, weledi na upendo baina ya uongozi wa TPDC na  wafanyakazi.

” Wizara ipo pamoja nanyi kuhakikisha azma na malengo makuu ya Serikali kwa TPDC yanafikiwa na zaidi”, Amesisitiza Mhe. Kapinga.



Aidha, amewakumbusha kuendelea kuyapa mkazo masuala yanayohusu wafanyakazi kwani ndio  kiungo muhimu cha kufanikiwa kwa mipango na malengo mbalimbali ya TPDC.

“Ni vema masuala yanayohusu motisha zao ikiwemo mishahara kuhuishwa inapobidi na kuboreshwa kama hali ya kifedha inaruhusu”, Amesema Mhe. Kapinga.


Ameongeza kuwa itasaidia kuwapa morali ya kuendelea kufanya kazi TPDC na kuvutia pia wafanyakazi wazuri sokoni.

Ametaka changamoto za wafanyakazi kukaimu nafasi za uongozi muda mrefu bila kuthibitishwa na changamoto za kupandishwa madaraja na nyinginezo zifanyiwe kazi ili kupunguza malalamiko kwa wafanyakazi.

About The Author

(Visited 29 times, 1 visits today)

Last modified: September 18, 2024

Close