Visit Sponsor

Written by 2:58 pm KITAIFA Views: 39

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUTOA ELIMU KWA JAMII KUHUSU OSHA

Mwanasheria mkuu wa Wakala wa Usalama wa afya mahala pa kazi (OSHA) Rehema Msekwa akizungumza katika mkutano huo.

Na Carren Mgonja

Waandishi wa habari nchini wametakiwa kutoa elimu kwa jamii juu ya shughuli za Wakala wa Usalama wa afya Mahala pa Kazi (OSHA).

Wito huo umetolewa Leo katika mkutano wa siku moja ulioandaliwa na Chama Cha Wafanyakazi wa vyombo vya Habari Tanzania (JOWUTA ) na Mtendaji mkuu wa mamlaka hiyo Hadja Mwenda.

Mwenda alisema wataendelea kushirikiana na JOWUTA kuhakikisha elimu ya masuala ya usalama wa afya mahala pa kazi inawafikia wafanyakazi na jamii kwa ujumla.

Mwenda alisema lengo kuu la semina hiyo ni kujenga uelewa kuhusu usalama mahala pa kazi kwa waandishi hao.

“Katika tathmini tuliyoifanya tumegundua kuwa kuna uelewa mdogo kwa wadau juu ya kazi zinazofanywa na Osha na kwamba ili kukuza uelewa huo tunapaswa kushirikiana na waandishi wa habari, na tumejipanga kuhakikisha elimu ya masuala ya afya mahala pa kazi inatolewa kwa kundi hilo kwani wanaamini kupitia waandishi wa habari itawafikia wananchi hasa wafanyakazi na wataelewa kwa undani zaidi juu ya usalama wa afya zao mahala pa kazi” alisema.

“Waandishi wa habari ni kundi muhimu na ndio
macho na masikio ya wananchi, ili liendelee kupata taarifa nzuri lazima liwe salama ndio maana tukasema jukumu letu tuwapatie elimu na wao waitoe hiyo elimu kwa jamii,” amesema

Mwenda amesema kupitia waandishi wa habari jamii itapata kuelewa kwa nini kuna sheria ya usalama mahala pa kazi na kusisitiza wanahabari wanaendelea kuwa nguvu kazi yenye afya inayofanya kazi kwa usalama.

“Tumetoa mafunzo haya ili waandishi wa habari nao wavitambue vihatarishi kwa sababu hakuna mazingira ya kazi ambayo hayana vihatarishi, kazi yetu sisi OSHA ni kuhakikisha vihatarishi hivyo havimuathiri mfanyakazi ili aweze kufanya kazi kwa tija hata akistaafu basi astaafu akiwa na afya njema,” amesema

Aidha amesema OSHA inapofanya ukaguzi mahala pa kazi inataka kuangalia namna ambavyo watu wanafanya kazi katika mazingira yanayotakiwa kwa mujibu wa sheria.

About The Author

(Visited 39 times, 1 visits today)

Last modified: August 21, 2024

Close