Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Mhe. Abdulrahman Kinana (kulia) akifurahia jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mbunge wa Ruangwa kwenye Mkutano Mkuu maalum wa CCM Wilaya ya Ruangwa leo Januari 2, 2024.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Mhe. Abdulrahman Kinana ameendelea na ziara yake ya kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye maeneo mbalimbali nchini na kufanikiwa kufika Wilaya Ruangwa mkoani Lindi.
Akiwa Mgeni rasmi kwenye Mkutano mkuu CCM Wilaya ya Ruangwa, Kinana ametoa salaam za Rais Samia kwa wakazi wa Ruangwa na kuwakumbusha WanaCCM utamaduni wa chama hicho wakati wa uchaguzi kwa Rais aliyepo madarakani.
Kinana amesema >>’Chama chetu kinaongozwa na Katiba, Kanuni na Utamaduni. Utamaduni tulionao CCM, Rais anapokua kwenye awamu ya kwanza tunapenda aendelee na kwenye awamu zinazofuata, Rais Samia yuko kwenye awamu ya kwanza, kwanini asiendelee kwenye awamu ya pili? Tuna sababu? hatuna. Kama kuna wengine watajitokeza kwenye vyama vingine katiba inaruhusu lkn kwa CCM hakuna wa kutuzuia Rais Samia asiendelee’ – Kinana.
Makamu Mwenyekiti Kinana ameyasema hayo baada ya kuombwa na Wajumbe wa Mkutano Mkuu maalum wa Wilaya Ruangwa.
Mkutano huo mkuu wa Wilaya ulihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi akiwemo Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa (Mb), Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hassan Ngoma na Viongozi wengine wa CCM.
About The Author
Last modified: January 2, 2024