Visit Sponsor

Written by 3:17 pm KITAIFA Views: 29

WANANCHI 761 WAPATA HUDUMA ZA UPIMAJI NA MATIBABU YA MOYO SIHA

Wananchi wa Siha wakijadili mambo mbalimbali huku wakisubiri
kufanyiwa vipimo vya moyo wakati wa kambi maalumu ya siku sita ya upimaji na
matibabu ya moyo iliyomalizika hivi karibuni katika hospitali ya Wilaya ya Siha.
Picha na: JKCI

Watu 761 wamepata huduma ya tiba mkoba ijulikanayo kwa jina la Mhe. Dkt.
Samia Suluhu Hassan Outreach Services kwa kufanya upimaji na matibabu ya
moyo katika kambi maalum ya matibabu iliyofanywa na wataalamu wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Wilaya
Siha. Kambi hiyo ilifanyika kwa muda wa siku sita kuanzia tarehe 18 hadi
23/12/2023 ambapo watu wazima na watoto walipata huduma ya matibabu.
Kwa upande wa watu wazima waliofanyiwa upimaji wengi wao walikutwa na
matatizo ya shinikizo la juu la damu, kutanuka kwa moyo, kuziba kwa mishipa ya
damu ya moyo na shida za valvu za moyo.

Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa jimbo la Siha Mhe. Dkt. Godwin
Mollel akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine na wataalamu wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) mara baada ya kumalizika kwa mbio za Siha
Marathon 2023 zilizofanyika hivi karibuni mkoani Kilimanjaro.


Watoto 55 walifanyiwa uchunguzi ambapo wengine walikutwa na matatizo ya
moyo ya kuzaliwa nayo ambayo ni matundu, valvu za moyo kuwa na shida na
kutanuka kwa kuta za moyo kupita kiasi.
Wagonjwa wengine kwa mara ya kwanza wamegundulika kuwa na matatizo ya
moyo ikiwa ni pamoja na valvu za moyo, kutanuka na kuziba kwa mishipa ya
damu ya moyo ambapo wagonjwa 66 tumewapa rufaa ya kuja kufanyiwa vipimo
zaidi na kutibiwa katika Taasisi yetu.
Katika kambi hii wananchi walipimwa vipimo mbalimbali vya moyo ikiwa ni pamoja
na urefu, uzito, kiwango cha sukari mwilini, kuangalia uwiano baina ya urefu na
uzito, kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography) na
kipimo cha mfumo wa umeme wa moyo (Electrocardiography) pamoja na vipimo
vya damu (utendaji kazi wa figo, ini na kiwango cha mafuta kwenye damu).
Tulikuwa na wataalamu wa lishe ambao walitoa elimu ya lishe bora ambayo
iliwapa wananchi uelewa wa kufuata mtindo bora wa maisha ambao utawasaidia
kuepukana na magonjwa ya moyo ambayo ni moja ya magonjwa yasiyoambukiza
na yanaweza kuyaepuka kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.
Katika kambi hii ya matibabu tumewajengea uwezo wataalamu wa afya wa
hospitali ya wilaya ya Siha ya jinsi ya kutambua na kutibu magonjwa ya moyo.
Tunawaomba wananchi muepuke tabia hatarishi zinazoweza kuharibu mioyo yenu
hii ikiwa ni pamoja na uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe uliokithiri. Zingatieni
mtindo bora wa maisha kwa kufanya mazoezi na kula vyakula bora.

About The Author

(Visited 29 times, 1 visits today)

Last modified: December 29, 2023

Close