Visit Sponsor

Written by 9:30 am KITAIFA Views: 63

WAKALA UAGIZAJI MAFUTA NCHINI: MFUMO UAGIZAJI WA PAMOJA UNAOKOA ZAIDI YA SH.BIL.500 KILA MWAKA

Na Beatrice Kaiza

MTENDAJI Mkuu wa Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Erasto Mulokozi amesema, Mfumo wa Uagizaji wa Pamoja wa Mafuta nchini (BPS) huwa unaokoa zaidi ya shilingi bilioni 500 kila mwaka.

“Kwa hiyo kwa wastani zaidi ya dola za Marekani milioni 200 sawa na shilingi bilioni 500 huokolewa kila mwaka kupitia mfumo wa BPS;
Mulokozi ameyabainisha hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika kikao kazi na wahariri wa vyombo vya
habari nchini chini ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Vile vile amesema, Mfumo wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja umeleta manufaa mengi ikiwemo uhakika wa upatikanaji wa mafuta yanayotosheleza mahitaji ya nchi na yenye viwango vya ubora unaotakiwa wakati
wote.

Sambamba na kupata unafuu wa gharama za uletaji wa mafuta (premium) kutokana na uagizaji wa pamoja.
Manufaa mengine, Mulokozi amesema ni kupungua kwa bei ya mafuta kutokana na uagizaji wenye ufanisi ikiwemo kuongezeka kwa mapato ya kikodi yatokanayo na bidhaa ya mafuta.

“Pia, mfumo umewezesha kupunguza vitendo vya ukwepaji kodi kutokana na udanganyifu uliokuwa unafanywa na baadhi ya waagizaji wa mafuta.”
Mulokozi pia amesema, mfumo umewezesha kudhibiti udanganyifu katika gharama za mafuta katika soko la Dunia na gharama za uletaji wa mafuta nchini.

Aidha, mfumo umewezesha kupunguza msongamano wa meli bandarini.
Katika hili, Mulokozi amesema wastani wa Dola za Marekeni milioni 170 sawa na shilingi bilioni 425 huokolewa kila mwaka ikilinganishwa na gharama za demurrage zilizokuwa zikilipwa kabla ya mfumo wa BPS.

Mtendaji Mkuu huyo ameomngeza kuwa, pia mfumo unatumika na nchi jirani katika ununuzi wa mafuta kwa nchi hizo.
“Hivyo kuipatia Serikali mapato kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya bandari. Kwa sasa uagizaji wa mafuta kwa ajili ya chi jirani umefikia wastani wa asilimia 55 ya kiwango cha mafuta kinachoagizwa kupitia BPS kutoka wastani wa asilimia 33 za awali.”

Jambo lingine amesema ni kupungua kwa upotevu wa mafuta wakati kwa kupakua mafuta kutoka melini ambapo wastani wa tani 1,100 sawa na lita 1,300,000 huokolewa kila mwezi (sawa na takribani shilingi bilioni 4.16 kwa bei kikomo za Desemba 2023″.

Mulokozi amefafanua kuwa,kwa mwaka takribani shilingi bilioni 49.9 huokolewa kupitia mfumo huo.

Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Jukwaa la
Wahariri Tanzania (TEF), Yasin Sadick ameipongeza mamlaka hiyo kwa kazi nzuri inayofanya kwa maslahi makubwa ya Taifa.

“Wengi wetu tulidhani PBPA ni kikundi cha Waarabu ambacho kimejikusanya na kuagiza mafuta hivyo kuiuzia Serikali, kumbe ni taasisi ya Serikali,hongereni sana kwa kazi nzuri.”

Aidha, ametoa wito kwa mamlaka hiyo kuendelea kushirikiana na vombo vya habari na wanahabari ili waweze kutoa taarifa za mara kwa mara kuhusu majukumu yanayofanywa na mamlaka hiyo nchini.

About The Author

(Visited 63 times, 1 visits today)

Last modified: December 12, 2023

Close