Kumekuwepo na wimbi la utapeli linalofanywa na watu wenye nia ovu ya kujipatia fedha kutoka kwa wananchi isivyo halali kwa kuweka matangazo katika mitandao ya Kijamii
kuwa wanatoa Namba za Utambulisho wa Taifa (NIN), Vitambulisho vya Taifa na
Nakala tepe mtandaoni (Online Soft Copy). Baadhi yao wametengeneza Akaunti
bandia (fake) za Mitandao ya Kijamii ya Mamlaka na hujitangaza kuwa wanatoa huduma
hizo kwa niaba ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na kuwataka wanaohitaji
huduma hizo kulipa fedha kupitia namba za simu za mkononi.
Tunawatahadharisha wananchi kujiepusha na watu hao kwani NIDA ndiyo taasisi pekee
yenye Mamlaka kisheria ya kutoa huduma hizo na haina wakala au mtu yeyote
inayeshirikiana naye kuchapisha na kutoa Namba na Vitambulisho vya Taifa. Aidha,
NIDA haina huduma ya Nakala tepe mtandaoni (Online Soft Copy).
Tunawakumbusha wananchi kuwa malipo kwa taasisi za Serikali ikiwemo NIDA
hufanywa kupitia Namba ya Malipo ya Serikali (Control Number) na si kupitia namba za
simu za mkononi hivyo, endapo mtu yeyote atakutaka kulipia huduma yeyote ya NIDA
kupitia namba ya simu ya mkononi, hayo si malipo halali ni UTAPELI.
Tunatoa rai kwa wananchi kutumia njia na taratibu sahihi zilizowekwa na Mamlaka katika
kupata huduma zetu za Usajili na Utambuzi ikiwa ni pamoja na kutumia ofisi zetu za
Usajili badala ya kutumia njia za mkato.
About The Author
Last modified: November 17, 2023