Visit Sponsor

Written by 12:01 pm KITAIFA โ€ข Views: 4

EWURA YAZITAKA MAMLAKA ZA MAJI KUWASILISHA TAARIFA SAHIHI ZA UTENDAJI WAO

Mkurugenzi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Mhandisi. Exaudi Fatael,akizungumza leo Novemba 15,2023 jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano wa Watendaji wa Mamlaka za Maji nchini.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imeziagiza Mamlaka za Maji za Mikoa na Miradi ya kitaifa kuwasilisha EWURA taarifa sahihi za utendaji kwa maendeleo ya sekta ya maji na taifa kwa ujumla.

Maagizo hayo yametolewa leo Novemba 15,2023 jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Majisafi na Usafi wa Mazingira Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Mhandisi. Exaudi Fatael, wakati akifungua Mkutano wa Watendaji wa Mamlaka za Maji nchini.

Mhandisi. Fatael, amesema EWURA imebaini uwepo wa baadhi ya takwimu zisizo sahihi kutoka mamlaka za Maji, hivyo imeitisha kikao hicho maalumu ili kuhakiki usahihi wa taarifa hizo.

 โ€œTakwimu hizi zinatumika kuandaa taarifa ya tathmini ya utendaji wa mamlaka za maji kwa mwaka 2022/23, hivyo ni vema kuhakikisha maboresho ya takwimu hizi yanaakisi uhalisia wa utendaji wenu.โ€amesema Mhandisi Fatael

Ameeleza kuwa baadhi ya takwimu zinazoboreshwa ni pamoja na takwimu za kiwango cha maji yanayozalishwa, muda wa huduma, usafi wa mazingira na ubora wa maji.

Naye Mhandisi. Joviyus Mabula kutoka Wizara ya Maji,amezitaka mamlaka za maji kuhakikisha zinatoa takwimu sahihi kwani Wizara hutumia takwimu hizo kupanga mipango ya sekta maji.

EWURA huandaa taarifa ya tathmini ya utendaji wa mamlaka za maji nchini kila mwaka kwa mujibu wa kifungu cha 29(2) cha Sheria ya Maji na Usafi wa Mazingira.

About The Author

(Visited 4 times, 1 visits today)

Last modified: November 16, 2023

Close