Visit Sponsor

Written by 6:13 pm KITAIFA Views: 63

MAKONDA: WATU WALIFUNGA USIKU NA MCHANA WAKIAMINI BADO NINA LA KUFANYA KWENYE TAIFA HILI

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Itikadi na Uenezi, Paul Makonda amesema kuwa akiwa kama msemaji wa chama hicho tawala sauti ya wanyonge itasikika kwakua wapo baadhi ya watu walifunga usiku na mchana wakiamini bado ana la kufanya katika Taifa hili wakiwemo wajane, wakina mama walemavu na makundi mbalimbali ambapo sauti yao ilisababisha tarehe 22, Oktoba 2023, jina lake likapata kibali tena katika Taifa la Tanzania.

Makonda ameyasema hayo leo Oktoba 26, 2023 katika ofisi ndogo za CCM, Lumumba Dar es Salaam wakati wa mapokezi yake kama mwenezi mpya wa chama hicho ikiwemo kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema kisha kuzungumza na maelfu ya wana CCM na wakazi wa Dar es Salaa waliofurika katika eneo hilo kumlaki.

“Namshukuru sana Mungu kwa afya njema na kuendelea kukipa Chama Cha Mapinduzi nafasi, zaidi kumlinda na kumtunza Mwenyekiti wetu wa chama Taifa, pia nawashukuru viongozi wa dini kwa faraja, wengine wakifunga usiku na mchana, kwa sauti yao na kilio chao wakiwemo wajane, walemavu na makundi mbalimbali. Na kwasababu hiyo nikiwa msemaji wa CCM chama tawala, chama kikongwe Afrika, chama cha pili kwa ukubwa duniani, sauti ya wanyonge itasikika,” alisema Makonda.

Aidha mwenezi huyo alisema kuwa hana kisasi kwa mtu yeyote na asiwepo yeyote akafiria lengo lake ni kumkandamiza, au kufikiria kuwa wakati huu atajitutumua kuonesha mabavu dhidi ya wale waliofikiria wamemtendea mabaya, bali anaamini Mungu aliwatumia kumsaidia kumjua Mungu zaidi kwani anaamini Mungu alimfanya kuwa mnyenyekevu zaidi na aliwatumia ili kumuandaa kwa kazi kubwa zaidi, wasiwe na hofu kwani kwake ni watumishi wa Mungu.

 “Kwa wale wataalamu wa maandiko wanakumbuka kazi aliyoifanya Farao kwa wana wa Israel, wanaosoma haraka biblia wanaweza fikiria Farao alikuwa mtumishi wa shetani, lakini Farao alikuwepo  kuchochea kusudi la Mungu dhidi ya wana wa Israel. Naamini nyinyi mlikuwepo kunisaidia ili nifikie mahala patakatifu kwa Mwenyezi Mungu. Naomba ushirikiano wenu na umoja wenu, wala Dkt. Samia hajaniteua kuja kuhangaika na mambo ya Makonda ameniteua kuhangaika na Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi, siyo kumtafuta mtu wa kwenda kulipa kisasi, bali walikaa kumtafuta mtu atakayeongeza nguvu katika kujenga imani ya Watanzania kwenye CCM,” alisema Makonda.   

Aidha Makonda amesema kuwa wanayo ilani yenye zaidi ya kurasa 300 ambayo jukumu lao ni kuitekeleza na kuieneza na kuwapa wanachi ili waamini kuwa chama chao kinafanyakazi kwa malengo na makusudi ya kuwakomboa na kuwaletea maendeleo. “Kwa hiyo kama kuna mtu amewaza Makonda atakuja na mambo gani, sina ya kwangu, ninayo ya Chama Cha Mapinduzi na hayo yanaongozwa na Dkt. Samia ambaye ndiyo mwenyekiti wetu na mtendaji mkuu ni Komredi Chongolo, kwangu mimi ni kupokea na kuja kuyasema kwenu na kuyatekeleza. Mimi kama nina mawazo nitayatoa kwenye sekretalieti na mwenyekiti wetu ni Chongolo ambaye ni mtu ninayemfahamu, nimefanya naye kazi nikiwa mkuu wa mkoa, yeye wa wilaya, anajua spidi yangu na uwezo wangu, nami najua upendo wake na uimara wake, kwa combination hii nina uhakika CCM itatoboa.

“Chama Cha Mapinduzi ni sikio la Serikali na sauti ya wananchi, kazi yetu ni kusikiliza kwa niaba ya Serikali na kusema kwa niaba ya wananchi, wanapokuwa na matatizo CCM inalojukumu la kusikiliza na kuyabeba kuyasema kwa Serikali, wananchi wakiwa na manung’uniko, huzuni ni jukumu la Chama Cha Mapinduzi kubeba huzuni yao, kubeba matatizo yao na kuiambia Serikali iyafanyie kazi. Naomba kutuma salamu kwa mawaziri wote, kwa wakuu wa mikoa akiwakilisha huyu hapa wa Dar es Salaam  wa Dar es Salaam, kwa watendaji wote kwamba pale patakapobainika hamjafanya kazi yenu kikamilifu chama hakitasita kuchukua hatua, bahati nzuri tunafahamiana.” Alisema Makonda.   

About The Author

(Visited 63 times, 1 visits today)

Last modified: October 26, 2023

Close