Visit Sponsor

Written by 2:17 pm KITAIFA Views: 22

UWEKEZAJI BANDARI DAR UNA TIJA KUBWA KWA WAFANYABIASHARA-MBWANA

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo, Martin Mbwana

Imeelezawa kwamba uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam utakapofanyika na kuongeza ufanisi katika utendaji wake utawarahisishia mambo mengi wafanyabiashara ikiwemo kuwapunguzia adha ya kwenda umbali mrefu kufuata mizigo.

Hayo yalibainishwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo, Martin Mbwana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana kuwa baadhi ya wafanyabiashara walikuwa wanakwenda kutoa mizigo Mombasa wakati Kariakoo na bandarini ni umbali wa kilometa moja.

“Mtu alikuwa yuko tayari kwenda kilometa 650, kupitia Horiri au kupitia Hororo ni umbali mkubwa zaidi, anaenda kutoa mzigo kule akijumlisha zile gharama anaona afadhari kutoa mzigo Mombasa, huyo ni Mtanzania na mfanyabiashara Kariakoo, anaacha Bandari ya Dar es Dalaam anaenda kule. Lakini pia utaona Kariakoo walikuwa wanaenda kununua mzigo Uganda na Uganda walikuwa wanapitisha mizigo hapa kwenye Bandari ya Dar es Salaam (Transit) inaenda mpaka Kampala, Watanzania wanatoka hapa wanaenda kununua mzigo Kampala, kwasababu ya ukiritimba uliokuwepo kipindi kile kupitia bandari ya Dar es Salaam,” alisema Martin.

Aidha mwenyekiti huyo alisema kuwa kitendo cha Rais Samia kuhamishia Serikali Dodoma na Dar es Salaam kuwa jiji la biashara imesaidia kulifanya jiji kufunguka, kila mahali ni wafanyabiashara, kitu ambacho kitaufanya uwekezaji wa Bandari ya Dar es Salaam uwe na tija kubwa kwao.

“Kwa hiyo sisi wafanyabiashara ili Dar es Salaam iwe ni kitivo au Dubai ya Afrika na Kariakoo iwe ni  Dubai lazima tukubali uwekezaji mzuri wenye tija, halafu sisi tuweze kufanya biashara kwa uhuru isiwe sababu ya mtu mwingine kusafiri nje ya nchi,” alisema.

Mbwana aliongeza kuwa uwekezaji Bandari ya Dar es Salaam hauepukiki kwasababu pia kuna miundombinu ambayo Serikali imeshaiweka kama Bandari Kavu ya Kwala, ambapo kuna miundombinu ya reli kutoka Dar mpaka huko, vilevile ujenzi wa reli ya treni ya kasi (SGR) ambayo inafungua kwenye mipaka ya jirani, pia miundombinu ya barabara ambazo zimefanywa na Serikali ya Awamu ya Sita inarahisisha kutoa mizigo kutoka bandarini kwenda nchi nyingine, kitu ambacho amesema hivi sasa ni muda muafaka kupata muwekezaji sahihi na kuendesha bandari kwa faida.

About The Author

(Visited 22 times, 1 visits today)

Last modified: October 20, 2023

Close