Visit Sponsor

Written by 1:24 pm KITAIFA Views: 8

WIZARA ZA KISEKTA ZATAKIWA KUCHUKUA HATUA SUALA LA EL NINO

Naibu Waziri Mkuu na Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko akimkabidhi Waziri wa Ardhi na Mbunge wa Ukonga Mhe. Jerry Silaa Mwongozo wa kubabiliana na madhara ya El nino leo katika kikao cha Mawaziri kilichofanyika JIjini Dodoma Leo Tarehe 13 Oktoba.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt Doto
Biteko ameelekeza kila sekta kuchukua hatua kwa
kuzingatia majukumu ya sekta husika katika suala zima la
utekelezaji wa mpango wa Taifa wa Dharula wa kukabiliana
ma Madhara yatokanayo na EL Nino.
Ameyasema hayo mapema Leo 13 Oktoba Jijini Dodoma
alipokuwa katika kikao cha wahemishimiwa mawaziri
kilichohusu Pamoja wa utekelezaji wa mpango wa Taifa wa
wa Dharula wa kukabiliana na Madhara yatokanayo na El
nino.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt Doto Biteko akizungumza wakati wa kikao cha wahemishimiwa mawaziri hawapo katika picha, kilichohusu utekelezaji wa mpango wa Taifa wa Dharula wa kukabiliana na Madhara yatokanayo na El nino,
kilichofanyika Jijini Dodoma jana 13 Oktoba 2023.

Baadhi ya maelekezo yaliyotolewa ni Pamoja na sekta
husika kuainisha na kuandaa rasilimali za kuzuia, kujiandaa
na kukabiliana na maafa endapo yatatokea kwa kila sekta
kushiriki kikamilifu katika eneo lake, na kutambua maeneo
hatarishi yenye viashiria vya kuathirika na maafa na
kuandaa mipango ya kuzuia madhara na kukabiliana na
maafa endapo yatatokea.

Aidha, Mhe. Bitekoe ameelekeza wananchi kuelimishwa na
kuhimizwa kuhama kwenye maeneo hatarishi na kutekeleza
shughuli za kiuchumi na kijamii katika maeneo salama
Pamoja na umuhimu wa kuweka akiba ya chakula na kulima
mazao yanayotumia maji mengi, kueleimishwa juu ya hatua
za kuchukua tahadhari ili kuokoa maisha na mali.

Pamoja hilo sekta husika zimetakiwa kuandaa na kutekeleza
mipango ya kuzuia milipuko ya magonjwa kwa binadamu,
wanyama na mimea.

Kwa upande Wake Waziri wa Nchi Anayeshughulikia
masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama,
alisema Pamoja na mambo mengine, Ofisi ya Waziri Mkuu
kwa kushirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania
iliandaa na kufanya Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa Hali
ya Hewa uliopokea Taarifa ya Mwelekeo wa Mvua za Vuli
(Oktoba – Desemba), 2023 kutoka Mamlaka hiyo, kujadili
madhara yanayoweza kutokea na kuainisha hatua za
kuchukua, tarehe 22 Agosti, 2023
“kushirikiana na Wizara za Kisekta, Ofisi Waziri Mkuu
imeandaa Mpango wa Taifa wa Dharura wa Kukabiliana na
Madhara ya El Nino kwa kipindi cha Septemba 2023 hadi
Juni 2024 kwa kushirikisha sekta husika na wadau.”
Alibainisha.

Waziri wa Nchi Nayeshughulikia masuala ya Sera Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati wa kikao cha Mawaziri kilichohusu utekelezaji wa mpango wa Taifa wa
Dharula wa kukabiliana na Madhara yatokanayo na El nino, kilichofanyika Jijini Dodoma Leo 13 Oktoba 2023.

Awali, akiongea katika Mkutano huo, Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa, Dkt. Ladslausi Chang’a
alisema kuwa tathmini ya hivi karibu inaonesha kuwa
matukio ya El nino yataongezeka kwa idadi na ukubwa wa
matukio kadiri ambavyo joto la dunia linavyoendela
kuongezeka.
“kama tulivyotoa utabiri mapema kuwa mfumo wa mvua za
vuli utachangizwa na mvua za El nino kwa mwaka huu wa

  1. Alisema.”
    Aliendelea kusema Mvua ya El nino ya mwaka huu 2023
    inaendana kwa mwenendo wake na El nino ya mwaka 1997
    na ya mwaka 2006, “Tofauti yake na ile ya 1997 ilikuwa na
    nguvu sana na iliendana na mfumo wa bahari ya hindi

ambao ulikuwa na nguvu sana hivyo, tunaendelea kufuatilia
mabadiliko katika bahari zote.” Alisisitiza.

About The Author

(Visited 8 times, 1 visits today)

Last modified: October 13, 2023

Close