Visit Sponsor

Written by 2:30 pm KITAIFA Views: 33

MKURUGENZI BANDARI DAR: HAKUNA MSONGAMANO WA ABIRIA KUTOKA ZANZIBAR

Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho akionesha moja ya Scanner zilizofungwa bandarini hapo (eneo la kushusha na kupakia abiria wanaotoka na wanaokwenda Zanzibar) ambazo zimeondoa msongamano kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa.

Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho ametolea ufafanuzi taarifa zilizoenea kwamba eneo la kupakia na kushusha abiria hasa wanatoka Zanzibar kuja Dar es Salaam limekuwa na msongamano mkubwa kwa sasa kitu ambacho amekikanusha na kuweka wazi ukweli ulivyo.

Akiongea na Waandishi wa Habari bandarini hapo leo Septemba 30, 2023 Mrisho amesema kuwa ni kweli changamoto hiyo ilikuwepo kipindi cha nyuma kwakuwa sasa kuna ongezeko kubwa la abiria wanaotoka Zanziba kuja Dar es Salaam na wanaokwenda Zanzibar, pia scanner ya kukagulia abiria ilikwa moja ndogo, lakini baada ya kufunga scanner mbili kubwa changamoto hiyo ikaisha.

Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Mrisho akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam jana Septemba 30, 2023

“Kipindi cha hivi karibuni kuliibuka taarifa kuhusu changamoto za eneo hili na hasa msongamano hasa wa abiria wanaoshuka kutoka Zanzibar kuja Dar es Salaam, niseme wazi kwamba hili eneo kwa siku tunahudumia abiria elfu 7 mpaka elfu 10, kwenye msimu kama mwezi wa 11, 12 na Januari yake tunaenda zaidi ya hapo kwasababu kunakuwa na abiria wengi wanaoenda na kurudi.

“Na tukumbuke eneo hili ndio watalii wetu wanapita kwenda Zanzibar na kutoka Zanzibar kuja Dar es Salaam, kwa hiyo ni eneo nyeti, kila siku unavyoendelea kuboresha huduma zako na changamoto pia zinatokea,” alisema Mrisho.

Aidha Mkurugenzi huyo alisema kuwa changamoto ya foleni hasa kwenye upade wa scanner, walitoa taarifa kwamba wameagiza scanner kubwa mbili, ambazo baada ya kuzifunga kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa hakuna tena tatizo la msongamano kwenye maeneo yote, hasa abiria wanashuka kutoka Zanzibar kuja Dar es Salaam.

“Kwa hiyo scanner mbili kubwa zenye uwezo mkuwa zimefungwa ili abiria wetu wasipate hiyo changamoto ya kukaa muda mrefu, kwa hiyo hilo tatizo la msongamano halipo hivi sasa, hilo ndilo ningependa Watanzania wenzangu wanielewe,” alisema Mrisho.

About The Author

(Visited 33 times, 1 visits today)

Last modified: September 30, 2023

Close