Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Septemba 24, 2023 amekagua uboreshaji wa miundombinu kwenye Chuo cha Ufundi Standi kilichopo kata ya Kijiji cha Bushagara, Kamachumu mkoani Kagera.
Maboresho ya chuo hicho yatagharimu shilingi milioni 903.5 ambapo mpaka sasa kiasi cha shilingi milioni 220.9 zimekwisha tumika.
Maboresho hayo yatawezesha ujenzi wa Bweni la wavulana, Bweni la wasichana, Bwalo la chakula , Karakana ya Umeme na Uchomeleaji, Nyumba ya Mkuu wa Chuo, pamoja na Jiko la kupikia chakula.
About The Author
Last modified: September 24, 2023