Visit Sponsor

Written by 10:03 am KITAIFA Views: 21

MAKAMU WA RAIS AZUNGUMZA NA DIASPORA NCHINI HUNGARY

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip
Mpango ameipongeza Jumuiya ya Watanzania waishio nchini Hungary pamoja
na Ubalozi wa Tanzania unaowakilisha nchini humo kwa msaada waliotoa
wakati wa kuwaondoa watanzania waliokuwa wakiishi na kusoma nchini
Ukraine mara baada ya kuanza kwa vita.
Makamu wa Rais ametoa pongezi hizo wakati alipokutana na kuzungumza na
Jumuiya ya Watanzania wanaoishi na wale wanaopata elimu ya ngazi
mbalimbali nchini Hungary, mazungumzo yaliofanyika Jijini Budapest nchini
Hungary. Amewataka kuendelea kushikamana na kushirikiana wakati wote na
kuwa na moyo wa huruma na upendo kama baadhi yao walivyojitolea hali na
mali kusaidia watanzania waliokuwa wakiondoka eneo la vita.


Makamu wa Rais amewasihi watanzania waishio nchini Hungary kuhakikisha
wanaishi kwa kufuata sheria katika nchi hizo na kujiepusha na vitendo vya
kihalifu vitakavyoharibu taswira ya Tanzania. Aidha amewaasa kuendelea
kuitangaza vema Tanzania, kuvutia wawekezaji pamoja na wao kuchangamkia
fursa za uwekezaji katika sekta mbalimbali nchini. Pia amewasihi kuendelea
kusaidia kwa karibu ndugu na jamaa wenye uhitaji katika familia zao nchini
Tanzania kwa kutumia mifumo rasmi ya utumaji fedha.

Halikadhalika Makamu wa Rais amesema kutokana na lugha ya Kiswahili
kuanza kutumika katika Jumuiya mbalimbali kama lugha rasmi, Diaspora
wanapaswa kuendeleza lugha hiyo kwa kuitangaza na kuanzisha vituo vya
kujifunzia lugha ya Kiswahili katika maeneo waliopo. Aidha amewataka
watanzania waishio nje ya Tanzania kutambua jukumu la kwanza la ujenzi wa
Tanzania litafanywa na watanzania wenyewe hivyo wanapaswa kutoa
mchango wa kila hali katika kuliletea taifa maendeleo.
Amewasisitiza wanafunzi kutumia fursa waliopata vema kwa kuvuna maarifa
na kutengeneza mahusiano mazuri na mataifa mengine ili kuweza kuijenga
Tanzania.
Makamu wa Rais amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais
Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuleta mabadiliko yenye tija kwa
watanzania wote na kueleza kwamba serikali imefanya jitihada katika
kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo afya, sekta ya elimu, kuimarisha sekta ya
nishati, ujenzi wa mindombinu kama vile barabara, reli viwanja vya ndege na
barabara. Pia amesema serikali inaendelea na jitihada za kuimarisha
demokrasia, sekta ya madini, maji na sekta ya kilimo kwa kuanzisha programu
za kuvutia vijana katika kilimo cha biashara.

Pia Makamu wa Rais amesema Serikali kwa kutambua ongezeko la watu
nchini imedhamiria kuwekeza katika kuimarisha rasilimali watu ili iweze
kutumika vema katika kuleta maendeleo. Makamu wa Rais amesema kwa
kuzingatia hali hiyo huduma za afya na elimu zimeboreshwa kwa kuongeza
vifaa tiba na miundombinu ya afya, kutoa fursa kwa madkatari kupata elimu
zaidi pamoja na ujenzi wa vyuo vya ufundi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Mbarouk Mbarouk amesema pamoja na kazi ya kukuza na kudumisha
mahusiano ya kirafiki na kidiplomasia kati ya Tanzania na mataifa mengine pia
serikali imeendelea kutekeleza kikamilifu kazi ya uratibu wa masuala ya
diaspora. Amesema kuanzishwa kwa mfumo wa kuwasajili diaspora kidijitali
(Diaspora Digital Hub) umesaidia katika kurahisisha kutambua takwimu za
watanzania waishio nje ya Tanzania.
Balozi Mbarouk amesema takwimu zitakazopatikiana katika mfumo huo
zitawezesha serikali kupanga na kuandaa kwa usahihi mahitaji yanayohitajika
ili kuwapa diaspora huduma wanazohitaji kama vile huduma za kibenki, hati
za kusafiria, vitambulisho vya taifa na vitambulisho rasmi vya utambuzi wa
diaspora wakati wa utekelezaji wa hadhi maalum.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanafunzi Watanzania
wanaopata Elimu nchini Hungary Michael Matonya ameishukuru serikali kwa
ufadhili wa wanafunzi wanaosoma nchini humo na kuomba kuongezwa kwa
idadi ya wanafunzi wanaosoma nchini humo hasa katika fani za kimkakati za
sayansi na teknolojia.
Pia ametoa wito kwa serikali kuwekeza zaidi katika kushirikiana na nchi ya
Hungary katika sekta ambazo nchi hiyo imepiga hatua kama vile na utaalamu
katika sayansi ya kompyuta, tehama, uhandisi, urubani, afya, elimu ya mimea
na wanyama. Kuongezwa kwa

About The Author

(Visited 21 times, 1 visits today)

Last modified: September 16, 2023

Close