Visit Sponsor

Written by 2:43 pm KITAIFA Views: 62

RAIS SAMIA AWATAKA WANASIASA KUTUMIA VYEMA UHURU WA KUTOA MAONI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na
Wadau wa Demokrasia kabla ya kufungua Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa Kutathmini Utekelezaji wa Mapendekezo ya Kikosi Kazi na Hali ya Siasa nchini. Mkutano huo umefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Septemba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa
wito kwa viongozi wa vyama vya siasa nchini kutumia mikutano ya hadhara kutoa
hoja na fikra zenye tija zinazolenga kuimarisha utendaji serikalini.
Rais Samia ametoa wito huo leo wakati akifungua mkutano wa Baraza Maalum la
Vyama vya Siasa kutathmini utekelezaji wa mapendekezo ya Kikosi Kazi uliofanyika
katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC).
Aidha, Rais Samia amevitaka vyama vya siasa kutumia mikutano ya hadhara
kujitangaza ili kukua kisiasa na kuutumia uhuru wa kujieleza kutoa mawazo mbadala
yatakayoendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa.


Rais Samia pia amesema uhuru wa kutoa maoni kusisababishe kudhalilisha watu
wengine, kuibua hisia za kidini, ukabila au kubaguana kwa misingi yoyote ile.
Vile vile, Rais Samia amesisitiza kutumia uhuru huo vizuri bila kuingilia haki na uhuru
wa watu wengine pamoja na kufuata sheria, kanuni na taratibu.
Kwa upande mwingine, Rais Samia ametoa wito kwa viongozi wa dini kwenye
maeneo yao kuisaidia serikali kurejesha maadili mema katika jamii.
Hali kadhalika, Rais Samia amesema kumekuwepo na mmomonyoko wa maadili,
udhalilishaji na ukatili wa kijinsia katika jamii ambapo vijana hufanya matendo yaliyo
kinyume na mila na desturi za Kitanzania.

About The Author

(Visited 62 times, 1 visits today)

Last modified: September 11, 2023

Close