Visit Sponsor

Written by 2:20 pm KITAIFA Views: 50

DKT. NCHEMBA ATUNUKIWA CHETI KUTAMBUA MCHANGO WAKE KATIKA SEKTA YA MAENDELEO NA UKUZAJI UCHUMI

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lamek Nchemba (Mb), (kulia) na Wziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Waimbaji wa Muziki wa Injili (Mapacha Watatu) Emmanuel, Zakayo na Marco Palangyo, baada ya hafla ya kumkabidhi mkandarasi, Kampuni ya Henan Highway Engineering Group Ltd, mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami, kutoka eneo la Sabasaba-Sepuka-Ndago hadi Kizaga, yenye urefu wa kilometa 77.6, utakaogharimu shilingi bilioni 88.6, hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Misigiri, Wilaya ya Iramba, mkoani Singida, jana.

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lamek Nchemba (Mb), (kulia) akipokea cheti cha kutambua mchango wake katika maendeleo ya mkoa wa Singida kutoka kwa Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa (Mb), wakati wa hafla ya kumkabidhi mkandarasi, Kampuni ya Henan Highway Engineering Group Ltd, mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami, kutoka eneo la Sabasaba-Sepuka-Ndago hadi Kizaga, yenye urefu wa kilometa 77.6, utakaogharimu shilingi bilioni 88.6, hafla iliyofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Misigiri, Wilaya ya Iramba, mkoani Singida, jana.

About The Author

(Visited 50 times, 1 visits today)

Last modified: September 11, 2023

Close