Visit Sponsor

Written by 3:43 pm KITAIFA Views: 98

SIMBACHAWENE AWATAKA WANANCHI KUPUUZA TAARIFA ZA UZUSHI KUHUSIANA NA NDEGE YA RAIS Gulf Stream (G550)

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali kabla ya kuzindua bodi hiyo jijini Dar es Salaam. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewataka wananchi
kupuuza taarifa za uzushi zinazosambazwa na watu wasio wema
kuhusiana na ndege ya Rais Gulf Stream (G550) kushikiliwa nchini
Dubai.
Mhe. Simbachawene ameyasema hayo leo wakati akizindua Bodi ya
Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali katika Kituo cha Kimataifa cha
Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
“Mtu anaweza kuzusha jambo na likawapotezea muda mwingi wananchi
badala ya kufanya mambo ya maendeleo, kwa mfano uzushi kuhusiana
na ndege ya Rais Gulf Stream (G550) kuzuiliwa Dubai, nataka
niwahakikishie Watanzania kuwa ndege hiyo ipo sehemu husika kwenye
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1 VIP, jijini
Dar es Salaam kwenye eneo ambalo Wakala wa Ndege za Serikali
wanalitumia na yeyote anayepita barabarani ataiona,” Mhe.
Simbachawene amesisitiza.
Mhe. Simbachawene amesema yeye akiwa ndiye Waziri mwenye
dhamana ya Utawala Bora ameona aliweke wazi jambo hilo, lililoleta
taharuki ili kuwaondoa hofu Watanzania na uvumi huo ulioenea, hivyo
lisiwapotezee muda wao na kuwahakikishia wanaovumisha hayo kwa
nia ovu wanaweza kwenda kupata uhakika wa uwepo wa ndege hiyo
ambapo ameongeza kuwa Viongozi wanasafiri kama kawaida kwa
kutumia ndege hiyo.
Aidha, Mhe. Simbachawene ametoa wito kwa Wajumbe wa Bodi hiyo
kushirikiana na Menejimenti ya Wakala wa Ndege za Serikali ili
kuiwezesha Wakala hiyo kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
“Ni matarajio yangu kuwa Bodi hii itasimamia vema utendaji wa Wakala
hii ili kuleta tija kwa maendeleo ya taifa kama inavyosisitizwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan,”
Mhe. Simbachawene amesisitiza.
Akitoa neno la shukrani, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa
Ndege za Serikali, Prof. Mhandisi, Idrissa Mshoro amemuahidi Mhe.

2

Simbachawene kuwa, yeye pamoja na Wajumbe wa Bodi hiyo kwa
kushirikiana na Menejimenti ya TGFA watatekeleza yote ambayo
ameyaelekeza kwani wanafahamu kwa kina maono makubwa ya Rais,
Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika katika kuharakisha maendeleo
ya nchi katika kuhakikisha uwepo wa usafiri madhubuti.
Kwa upande wake, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za
Serikali (TGFA) Capt. Budodi Budodi amesema Menejimenti ya Wakala
inamhakikishia Mhe. Simbachawene kuwa wataendelea kutekeleza
majukumu yao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu pamoja na
maelekezo ya Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali ili kufikia
malengo ya uanzishwaji wa Wakala hiyo.

About The Author

(Visited 98 times, 1 visits today)

Last modified: August 25, 2023

Close