Visit Sponsor

Written by 6:00 pm KITAIFA Views: 25

RAIS SAMIA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI WA MIKATABA YA MSAADA WA MAENDELEO INAYOFADHILIWA NA EU

Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, akishuhudia kusainiwa kwa mikataba mitatu yenye thamani ya shilingi bilioni 455.09 na msaada wa shilingi bilioni 117.04 kwa ajili ya utekelezaji wa Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/2023, katika Ukumbi wa Hazina (Treasury Square), jijini Dodoma. Kwa upande wa Serikali ulisainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (kulia) na Balozi wa Umoja wa Ulaya Nchini Tanzania, Mhe. Manifredo Fanti. Anayeshuhudia upande wa kushoto ni Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan
ameshuhudia utiaji saini wa Mikataba 3 ya msaada wa maendeleo inayofadhiliwa na
Umoja wa Ulaya (EU) wenye thamani ya Euro milioni 179.35 sawa na Shilingi bilioni
455.09 za Kitanzania.
Aidha, Rais Samia ameshuhudia kutangazwa kwa fedha za msaada wa bajeti ya
Serikali zilizotolewa na EU kiasi cha Euro milioni 46.11 sawa na Shilingi bilioni
117.036 za Kitanzania kwa mwaka wa fedha 2022/ 2023.
Fedha hizo zitaelekezwa katika sekta za maendeleo hasa katika uchumi wa Buluu,
uwezeshaji wananchi kiuchumi pamoja na uimarishaji mifumo ya ukusanyaji na
usimamizi wa fedha serikalini.
Katika hafla hiyo iliyofanyika ukumbi wa Hazina Rais Samia ameishukuru EU kwa
kuwa msaada huo ni matokeo ya ziara aliyoifanya Brussels, Ubelgiji alipokutana na
Rais wa Tume ya Ulaya Mhe. Ursula Von der Leyen.
Msaada huo uliotolewa kwa Serikali unaendana na mipango mkakati ya kisekta na
maendeleo nchini, hususan Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano, Dira
ya Maendeleo ya Tanzania 2025 na Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2050.
Aidha, Rais Samia amesema Programu hizo pia zitaendana na kaulimbiu ya Mwaka
wa Fedha wa 2023/24, kama ilivyopitishwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC):
“Kuongeza kasi ya kufufua uchumi, kukabiliana na kupunguza mabadiliko ya
tabianchi pamoja na kuimarisha sekta zenye tija kwa maisha bora”.

About The Author

(Visited 25 times, 1 visits today)

Last modified: July 4, 2023

Close