Visit Sponsor

Written by 4:25 pm KITAIFA Views: 39

BANDARI KIGOMA YAHUDUMIA TANI 131’000 MPAKA KUFIKIA MEI 2023

Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Edward Mabula akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani)

Bandari kongwe ya Kigoma iliyopo kunako eneo la Ujiji imeendelea kufanya vizuri katika upande wa upokeaji na usafirishani shehena mbalimbali kwa kuhudumia tani 131’000 kwa kipindi cha Julai 2022 hadi Mei 2023, sawa na asilimia 48 ya mzigo wote ambao unahudumiwa na ukanda wa Ziwa Tanganyika.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Juni 2, 2023 Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Edward Mabula amesema kuwa ukanda huo wa Ziwa Tanganyika ambao una bandari takribani 18 kwa ujumla umehudumia tani 273’ 000 mpaka kufikia Mei 2023.


“Tunaamini ufanisi ni mzuri na bado utaendelea kuongezeka. Nikizungumzia kuhusu Kigoma, ipo katika mchakato wa kuiboresha zaidi, upembuzi yakinifu umeshafanyika kupitia mtaalamu elekezi kutoka Uholanzi tangu 2017 wakaona kuna haja ya kukarabati Bandari ya Kigoma, na wenzetu Shirika la Maendeleo la Japan, wameonesha nia ya kufanya hii shughuli, sasa hivi ukarabati huo upo katika hatua za ununuzi kwa maana ya kumpata mkandarasi. Tunategemea kuanza ukarabati huo mwezi wa 9 mwaka huu,” alisema Mabula.


Aidha meneja huyo alisema kuwa, kwa ukanda huo wa Halmashauri ya Ujiji pia kuna bandari nyingine mbili ambazo zipo katika ukarabati mkubwa, Kibirizi ambayo inakarabatiwa kwa gharama ya shilingi bilionui 16.4 na ile ya Ujiji kwa gharama ya shilingi bilioni 7 ambapo ukarabati huo umefikia asilimia 68 mpaka 70 na matarajio ni kwamba, ukikamilika mizigo kwa maana ya shehena itaongezeka pamoja na mapato.
“Bandari ya Kibirizi ni maalum kwa ajili ya abiria ambapo wengi wanakwenda DRC Kongo, Ujiji pia mizigo yake mingi inakwenda bandari za ndani, matumaini ni kwamba baada ya kukamilika kwa bandari hizi, mapato na huduma nyingi za bandari za Ziwa Tanganyika zitaongezeka na zitaboresheka,” alisema.
Meneja Mabula alisema kuwa, bandari kongwe ya Kigoma iliyopo ndani ya Ziwa Tanganyika lenye urefu wa mita 4,470 ilijengwa na Wabeligiji mwaka 1922 na kuanza kazi 1927. “Ziwa Tanganyika linaikutanisha Tanzania na nchi za DRC Kongo, Burundi na Zambia, pia limetawanyika katika mikoa mitatu, Rukwa, Katavi na Kigoma.

About The Author

(Visited 39 times, 1 visits today)

Last modified: June 3, 2023

Close