Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, ametoa wito kwa Watanzania kutumia nishati mbadala kwa lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Serikali imeunda kamati ya kitaifa kutoa elimu na kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala. Waziri Mkuu pia amewataka wajasiriamali kutumia rasilimali za ndani kuzalisha nishati mbadala. Amesifu jitihada za Wakala wa Umeme Vijijini (REA) katika kupeleka umeme vijijini na kuwataka wahakikishe kila kijiji kinapata umeme.
“Wale mliopewa jukumu la kusimamia hili, jiridhisheni na kuhakikisha kila kijiji kinapata umeme, na muwasimamie wakandarasi ili wafanye kazi hiyo kikamilifu.” Amesema Waziri Mkuu
Kwa upande wake, Waziri wa Nishati Januari Makamba amesema wizara hiyo imejipanga kutumia makundi mbalimbali katika kuhamasisha Watanzania juu ya matumizi ya nishati mbadala.
“Pamoja na hili Wizara fikapo Julai 2023 itazindua dira ya Nishati Safi ya kupikia”
About The Author
majaliwa makamba waziri mkuu waziri wa nishati
Last modified: May 30, 2023